Mkutano wa kocha Frank Lampard hii leo kabla ya mechi ya kesho ambapo Chelsea itakuwa ugenini kuikabili Crystal Palace.
“Kante hatokuwepo kwenye kikosi kutokana na majeraha ya nyama za paja. Kovacic amefanya mazoezi ingawa ataukosa mchezo pamoja na Tomori nategemea anaweza kurejea wiki ijayo.”

Kama ushindi wa jumamosi umeirudisha Chelsea kwenye njia;
“Sidhani kama tulikuwa nje ya njia. Kila mechi ni ngumu. Crystal ni timu ngumu pia iliyojipanga zaidi kwenye kuzuia hivyo tunatakiwa kuchagua njia sahihi ya kuukabili mchezo.”
Kama Man utd ni mpinzani mkubwa kwa Chelsea;
“Ni mpinzani mkubwa kutokana na aina ya kikosi walichonacho. Wachezaji wake watatu wa mbele wote wanafunga magoli mengi na wana hali ya juu. Ni wapinzani wakubwa lakini kinachotakiwa zaidi ni jinsi gani utamaliza msimu.”
Kuhusu kurejea kwa Loftus-Cheek na Hudson-Odoi;
“Kwa Loftus-Cheek hiki ni kipindi chake muhimu cha kurejea mchezoni na kujiweka sawa lakini msimu ujao ndicho kipindi atakuwa kwenye ubora zaidi. Lakini hiyo haimaanishi kama kwasasa hawezi kuwa bora.”

“Ni hivyo hivyo kwa Callum pia, lakini yeye anatakiwa kuhakikisha anafanya mazoezi kwa bidii sana ili azidi kuwa vizuri. Kwasasa tunaona kile ambacho Pulisic na Willian wanakifanya, basi vile ndivyo anatakiwa kufanya Callum au ata kwa ukaribu wake.”
Kuhusu Jorginho kuziba pengo la Kante;
“Ni mchezaji mzuri. Na anataka sana kucheza na hilo kila mchezaji analitaka. Na mara zote amekuwa akifanya mazoezi vizuri. Kila mchezaji ana umuhimu wake tofauti ipo kwenye uchaguzi wa kikosi tu. Na sitaki kuelezea sababu ya kwanini nimechagua uyu acheze ama yule asicheze. Muhimu zaidi ni kutambua wachezaji wote ni machaguo yangu.”

Tofauti ya Eden Hazard na Christian Pulisic;
“Kwakuwa nimewai kucheza na Hazard, namtambua kama mchezaji mwenye kipaji kikubwa ambaye anaweza kuwavuta mabeki wamkabe yeye uku akitengeneza nafasi kwa wengine. Wakati Pulisic ni mchezaji zaidi anayetazama mbele, kitu ambacho nakipenda.”

“Ni aina ya mchezaji akipata mpira atapambana kuhakikisha anavunja mhimili wa mabeki kisha anashambulia. Ukizungumzia kuwalinganisha kwa hapo nitakaa pembeni. Hazard ameshakuwa hapa na amefanya makubwa.”


Hope mwaikuka
Namkubal sana Lampard
Saupha mohamed
Mechi itakua bombo sana
Povel
Don’t miss Pulisic & Zaha
Issa
Ni mechi ngumu sana kwa chelsea sababu crystel wana zaha ambae ni msumbufu eneo la penati
Saupha mohamed
Mechi itakua bombs sana
Sabrina
Maoni:kukosekana kwa kante itawapa ugumu chelsea kwa kiasi fulan hivi
neema hassan
Hii si yakukosa
Theckla
Itakuwa hatari sana
Furahav
Leo patachimbika.
Omary lukumbi
Lampard ni kocha mzr na anaijua.vzr Chelsea ila atakua na kibarua kizito
Njiku
Patachimbika hapo maana wote wanatetea nafasi zao
fatumakasom
Itakua poa
Theonestina
Siwezi kukosa pesa
Shafii
Ni mechi ngumu Sana ila kwa Chelsea wanapaswa kushinda hii mechi kujiakikishia nafasi nzuri ya top 4 ili washiliki club bingwa msimu ujao.
Samiah
Cyakukosa hii mechi
Franky
Kibabae sanaa
Hamidu
Chelsea mpo vizuri
Neema juma
Itakuwa poa sanaaa
Latifa juma mohamed
Mechi ya kibabe.
Rehema
Mechi kali
Amani
Wameponea chupu chupu kutoa draw# meridianbettz
Caroline
Sawa tu.
Asia Abdy
Mechi ilikua kal
warda
Bora Angekuwepo Kante ila wanaweza kushinda #Meridianbettz
Adelta
Hii sio ya kukosa
Mwanahamisi
Mechi utakuwa ya kibabe
Ester jackson
Mechi ngumu sana ila kwa Chelsea wanatakiwa kushinda kujiweka katika nafasi zaidi nzuri kwao
Magdalena
Lampard namkubali Sana anajituma na anajua Nini anafanya
felister
sidhani km Chelsea anaweza shinda iyo mechi
David Pere
Mechi ilikuwa inaonyesha lazima Chelsea washinde ili wajiweke sehemu nzuri ya kiwepo nne bora
Dorophina
Lampard najua ameiandaa vizuri sana timu yake
isha
Lampard namkubali sana
Genia Sikaluzwe
Mechi Kali Sana hii siwezi kukosa kabisa
Samira
Chelsea lazima ashinde
Evaluziga
Namkubali Sana lampard
Salma
Leo patachimbika
Khadija
duuh mpira uwanjani tutaona nani mkali kwa mwezie#meridianbettz
devotha
Lampard ni kocha mzuri sana
Isaya massawe
Lampard anakuja vizuri
Lydia Emmanuel Magoti
Lampard yupo vizuri
Ernest
Pulisic ni bonge la mchezaji