Ulaya: Immobile Mfalme Mpya

Msimu huu (2019-20) umekuwa wa aina yake kunako anga la soka barani Ulaya. Mbio za kutafuta tuzo za kiatu cha dhahabu hakika zilikuwa za kusisimua ukimtizama Ciro Immobile na nyota wengine.

Tuzo hiyo hutolewa kwa mchezaji aliyefunga magoli mengi katika Ligi tano kubwa barani Ulaya – EPL, La Liga, Serie A, Bundesliga na Ligue 1.

Msimu huu umekuwa wa aina yake kwa wachezaji mbalimbali kuonesha uwezo wao katika kupachika magoli. Ciro Immobile anaekipiga kunako timu ya Lazio inayocheza Serie A amekuwa na msimu mzuri kwa kupachika jumla ya magoli 36 katika michezo 37 aliyocheza msimu huu.

Ulaya
Ciro Immabile akishangilia goli

Lionel Messi wa Barcelona kunako La Liga amefunga magoli 25, Cristiano Ronaldo (31) na, Lewandowski (34). Katika idadi hizi, Immobile amefunga magoli 14 na Ronaldo 12 kwa mikwaju ya penati, Messi amefunga magoli 5 kwa mipira ya faulo wakati Lewandowski akifunga penati 5 pekee.

Akizungumzia mafanikio hayo, Immobile amenukuliwa akisema ” Inashangaza, mimi kuwa kati ya Ronaldo na Lewandowski. Nikiangalia orodha ya waliotangulia siamini, ni Messi, Messi, Suarez, Ronaldo, Ronaldo, Messi, Messi, Ronaldo, Messi”

ulaya
Messi akiwa na tuzo zake zote za mchezaji bora wa Ulaya

“Nimeingilia utawala wa Messi na Ronaldo. Kwa hili, ninawashukuru wachezaji wenzangu”

Kwa idadi ya magoli ya Immobile msimu huu, ameifikia rekodi ya Gonzalo Higuain ambaye alifunga magoli 36 katika msimu mmoja wa Serie A mwaka 2015-16.

ulaya
Cristiano Ronaldo na tuzo yake ya 5 ya mchezaji bora duniani

Pamoja na hilo, Immobile pia amezungumzia taarifa ya David Silva kujiunga na Lazio msimu ujao. Kumekuwa na taarifa kwamba kiungo huyo ananafasi kubwa ya kutimkia Serie A baada ya kuitumikia Manchester City kwa miaka 10.

ulaya
David Silva

Kuhusu ujio wa Silva, Immobile amesema ” Ni mchezaji mzuri mwenye uzoefu mkubwa, tunasubiri kumpokea kwa mikono miwili. Ninashauku kubwa ya kumpokea, sisi ni mashabiki kabla ya kuwa wachezaji wa Lazio”.

Pamoja na mafanikio ya Immobile msimu huu kunako Serie A, timu anayoingoza kama Nahodha – Lazio, wamemaliza ligi katika nafasi ya nne nyuma ya mabingwa Juventus, Inter Millan na Atalanta.


Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.

soma zaidi

40 Komentara

    Hongera immo

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Congrat immobile Ciro 🤝🤝🤝🤝

    Jibu

    Hongera sana immobile

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Immobile ni moto sana

    Jibu

    Immobile hajataka masihara msimu huu

    Jibu

    Baada ya mafanikio haya nilitegemea vikumbo vya timu kubwa vianze kumunyatia#meridianbettz

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Habar njema sana 👍

    Jibu

    Hongera Imobile unatamba wewe tuuu!!!!

    Jibu

    Immobile amefanya kitu kikubwa Sana kwenye ligi hiyo amempiku hadi cr7 kwa magoli.

    Jibu

    Safi🤙

    Jibu

    Hongera immobile msimu huu hukutaka kulala

    Jibu

    Good news
    @meridianbettz

    Jibu

    Safii

    Jibu

    Immobile ajataka mshahara mwezi huu#meridianbettz

    Jibu

    safi

    Jibu

    Safii

    Jibu

    Immobile anadeserve.

    Jibu

    Tunzo za safari hii kumekua na mabadiliko makubwa sana toka mapunziko ya korona wachezaji wamekua na molali makubwa sana kimichezo

    Jibu

    Amestahili sanaa

    Jibu

    Pongezi nyingi kwake mana nilitegemea majina ambayo tumeyazoea sasa ni zamu ya wengine

    Jibu

    Kafanya vizuri sana immobile kavunja rekodi safii sana isihishie hapa kwa immobile andelee kushindana

    Jibu

    Pongezii kwa immobile!!!

    Jibu

    Pongezi kwake

    Jibu

    Pongez kwake

    Jibu

    Anastahili pongezii Kwa kweliii

    Jibu

    Immobile amekuja kufanya Jambo zuri mbele ya cr7 anastahili pongezi.

    Jibu

    Hongera sana immobile

    Jibu

    Hongera immobil

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Hakika yuko vizuri immobile

    Jibu

    Safi sanaa

    Jibu

    Safii

    Jibu

    safi sana

    Jibu

    Hongera yake

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.