Ripoti zinazochanja mbuga kwa kasi kule Uingereza ni kuwa klabu ya Chelsea inataka kufanya dili la mabadilishano kati ya mlinda mlango wake Kepa Arrizabalaga ili kumpata golikipa Gianluigi Donnarumma wa Milan.
Mkataba wa sasa wa mzuia mikwaju Donnarumma pale San Siro unaisha mwaka 2021, na kwa mujibu wa wakala wake Mino Raniola mpaka sasa hakuna maongezi yaliyofanyika kumuongezea mkataba.
Sababu ya kutofanyika kwa mazungumzo ya kusaini mkataba mwingine inatajwa kuwa ni kwa sababu klabu ilikuwa ‘bize’ na suala la mkataba la Zlatan Ibrahimovic, mazungumzo ambayo yamekamilika wikiendi hii na dili linatarajiwa kuwa litasainiwa Jumatatu.
Bada ya ishu ya Zlatan, sasa Milan wanaweza kurejea kwa Donnarumma kuhakikihsha kuwa hataondoka kama mchezaji huru msimu ujao.
Hata hivyo, taarifa zinataja kuwa klabu ya Chelsea ilikuwa inafanya mazungumzo na Donnarumma, na wapo tayari kumtoa Kepa na kiasi cha pesa ili kumnasa golikipa huyu mwenye miaka 21.
Kepa ambaye sasa anatimiza miaka 26 Oktoba, alinunuliwa kwa €80m katika msimu wa joto wa mwaka 2018, lakini hivi karibuni amekuwa akiachwa kikosini kwa sababu ya makosa kadhaa.
Hata hivyo, vyanzo vya habari vya Italia havizungumzii kwa upana suala hili. Inawezekana Milan wakahitaji kusalia na Donnarumma.
Beti Mbio za Mbwa Mubashara
Hii ni rahisi zaidi! Hapa USHINDI unaupata kwa kuchagua mbwa anayeshinda mbio na machaguo mengine yenye odds tamu.


JULIANA
Asante kwataharifa
Lydia Emmanuel Magoti
Kama nivyo nivizuri mwendo wakupiga pesa tuu hapo
Dorophina
Hilo bonge la dili la maana kwa klabu hizo mbili
Mwajumah
Asante kwa makala
Caroline
Hapana Kepa ni level nyingine..
magdalena
chelsea wakisema wamtoe kepa watakuwa wamekosea sana maana kepa ana msaada mkubwa sana pale
Theonestina
Asanteni meridianbet kwa taarifa nzuri
lombo
habar njema
aisha
Itakuwa powa sana kama chelsea wakimpata Gianluigi donnarumma wa milan
Issa
Kama kepa kashafungashiwa virago the blues
Sadick
Hii ni fursa kwa wakala mwenye makeke mengi Mino Raiola kutengeneza pesa kama kawaida yake, sidhani kama AC Milan itakuwa tayari kumupoteza golikipa wao namba moja#meridianbettz
Genia Sikaluzwe
Habari njema
Hope mwaikuka
Inawezaka tu
Shafii
Chelsea kwa sasa kiu yao kubwa ipo kwa mlinda mlango ipo tayari kufanya lolote kupata mlinda mlango mwengine kwa ajiri ya msimu ujao.
Amiri Kayera
Dah saiv wanatak kumtoa chambo
Rose kapinga
Wafanye chaguo sahihi maana hawachelewi lawama kurudisha kwa kipa!!!
Ester jackson
Kama hili dili likikubaliwa na Milan basis Chelsea watakuwa wameokota dodo kwenye mnazi .
Njiku
Hahahaha Chelsea wamemchoka kipa wao arrizabalagakama man u walivyomchoka de gea kwa kufungwa magoli ya kizembe
Frank P
Milan wasijiroge kumuachia golie wao
neema hassan
Gud newz
Devotha
Habari nzuri
felister
dili la maana
Fatina mfigi
Mmmh
Ernest
Utoto umemponza Kepa na tamaa ya kuwa bora ghafla bila kujifunza zaidi kutoka kwa wakongwe, Binafsi namuona kama kipa hodari tena kijana sema anatakiwa kujifunza kitu juu ya nidhamu na kujenga kitu kinaitwa team work katika maisha yake ya soka.
Nasra
Asantee kwa taarifa
Rehema
Iko poa
Saupha mohamed
Habari njema
Asia Abdy
Wasimuache kepa
Sabrina
Chelsea wajitahidi wampate atawafaa
Janeflora malisa
Habar njm
Zeiyana
Chelsea kama wakipata saini ya mlinda mlango huyo tayali watakua washaimarisha kikosi chao so tumeona kwenye usajiri wao wamefanya vizuri sana
Sauda
Dili bomba
warda
Chelsea wangemchukua huyu ingekuwa poa sana
Johnmary joel
Itapendeza sana kama chelsea watampata#meridianbett
David Pere
Chelsea kwa sasa kiu yao kubwa ipo kwa mlinda mlango ipo tayari kufanya lolote kupata mlinda mlango mwengine kwa ajiri ya msimu ujao.
Gabriel
fursa kwa wakala mwenye makeke mengi Mino Raiola kutengeneza pesa kama kawaida yake, sidhani kama AC Milan itakuwa tayari kumupoteza golikipa wao