Liverpool hawajafanya maingizo yoyote mapya kwenye kikosi chao zaidi ya Kostas Tsimikas, beki wa kushoto kutoka Ugiriki, si usajili unaofikirisha. Tunajua anakuja kumsubiri Andy Robertson, ila si kuingia kwenye kikosi cha kwanza.
Bado ukisoma magazeti kutazama tetesi za usajili, Liverpool wao hawapo. Taarifa yao ni moja tu, Thiago Alcantara, hakuna mwingine na dili la Alcantara litafanikiwa tu iwapo Giorgio Wijnaldum atajiunga na Barcelona.
Hii inamaanisha nini? Klopp anaamini anaweza kwenda kutetea taji lake na kikosi kilekile kilichotwaa taji msimu uliopita. Ndiyo maana hajihangaishi sokoni. Swali linakuja, Je ni kweli Liverpool wanaweza kutetea taji na kikosi kilekile?
Kwa haraka, akilini kwetu ni kitu kisichowezekana, haswa tukitazama usajili walioufanya Chelsea na Man City. Zaidi ya yote, tunaamini Liverpool wamechoka, wametumia kikosi hichohicho kwa miaka mitatu. Watasumbuliwa na ‘fatigue’ na kisaikolojia hawapo kimapambano. Kwanini? Walifika fainali ya UEFA, msimu uliofuata wakachukua, wakawa wa pili kwenye ligi, msimu uliofuata wakachukua ligi. Unadhani wanahitaji nini tena? Hakuna. Hivo hawawezi kuwa na ari kama waliyokuwa nayo misimu mitatu nyuma.
Hizi ni hoja za msingi, tena zina mashiko. Ila nilikuwa na mawazo tofauti kidogo. Mimi binafsi yangu, ninaamini Liverpool wanaweza kulitetea taji lao. Kwanini?

Kwanza sidhani kama Liverpool inahitaji sura mpya sana. Sioni eneo ambalo Liverpool wana udhaifu. Kuanzia golini mpaka mbele. Liverpool wanakosa kikosi kipana tu, ila hawakosi wachezaji bora. Isitoshe Minamino na Keita hawakutumika msimu ulioisha, uwepo wao ni sawa na usajili mpya.
Pia wachezaji wengi wa Liverpool wapo katika umri wa kuwa kwenye peak. Tukimuacha TAA mwenye miaka 21. Wengi wapo katika umri wa kuwa kwenye moto. Hili linatokea wakiwa wamecheza pamoja kwa muda mrefu. Hawahitaji muda tena kuzoeana.
Mwisho tusisahau kuwa kocha wao ni Jurgen Klopp. Mtu aliyefanya visivowezekana viwezekane. Aliifikisha Dortmund mbovu fainali ya UEFA, akachukua nayo Bundesliga. Ameigeuza Liverpool kuwa tishio kwa mikakati tu. Tusisahau huyu ni Klopp.
SHINDA NA MERIDIANBET!
Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.


Johnmary joel
Ni kweli kikos cha liverpool siyo kibaya.hadi kocha wao chamsingi wachezaji wajipange vizuri msimu mpya#meridianbett
Adelta
Hapa kazi ipo tusubiri tuone@meridianbettz
Dorophina
Klopp anajiamini na kikosi chake kwamba kinaweza kumletea tena ushindi msimu huu unaoanza
felister
Klopp anaamini anaweza kutetea tena taji lake kwa kikosi kile kile
sylvester
Liverpool bado wana timu kubwa sana ambayo haihitaji marekebisho makubwa vinginevyo labda kuwe na mchezaji anataka kununuliwa
Mwanahamisi
Klopp anaamini anaweza kutetea
Sauda
Klopp yupo vizuri sana
Sadick
Klopp aliimarisha Liverpool kwa awamu ,msimu ulipoisha aliangalia pengo lipo wapi na kufanya usajiri kulingana na mahitaji#meridianbettz
Mwajumah
Klopp anajiamin sana na kikosi chake#Meridianbettz
Caroline
Hii inamaanisha klopp anawaamini wachezaji wake
Janeflora malisa
Klopp yup vzr
Ernest
Sina mashaka na kikosi cha Liver lakini najuwa watakutana na changamoto nyingi lakini bado wananafasi kubwa ya kutetea ubingwa
warda
Kikosi chake kipo poa hata asipo badilisha#Meridianbettz
Rose kapinga
Hatutaki maneno yake,tunasubiri vitendo!!!!
rama
klopp bado hanakiamini kikosi chake kama bado kipo vizuri
mwakalosi
katika makocha wa sasa ni klopp pekee unayeweza kumpa aston villa na bado akaleta ushindani mkubwa
Issa
Kloop ana kikosi bora sana ila inabid awe na kikosi kipana zaid sana kwakuwa kama
Akitumia kikos kimoja wachezaji watachoka
Sabrina
Klopp kikosi chake kikoimala
Theckla
Kolopp ni kocha mzuri sana pia kikos chake kipo vizuri sana
Mariam mtandama
Habari njema
Tatu
Liverpool bado wapo imara na kikosi chao kile kile na bado wanafanya vizuri kwenye soka
JULIANA WILBARD ALEX
Safi
Khadija
klopp yupo vzr sana#meridianbettz
Furahav
Liver bado iko gud.
Nasra
Liverpool bdo ipo vzuri
lombo
asante meridianbet kwa habar moto moto
Edgar
Nakubali
Shani
Kloop ana Kikosi kilicho bora na inabidi a badili Kikosi kwakua Kikosi alichonacho kitachoka kwa msimu ujao
Gabriel
Klopp ni kocha mzuri sana
Theonestina
Safi
Saupha mohamed
Klopp namwamini sana
Samira
Klopp ni kocha mzuri sana na anauwezo mkubwa sana
Neema
Habari njema
Shafii
Super manager.
Samiah
Klopp ni kocha mzuri
Amiri Kayera
Me naon Liverpool inafany usajir wa akili
Magdalena
Klopp aache kufanya mambo kwa mazoea nyakati ubadilika
aisha
Kikosi cha klopp kimejipanga ipasavyo