Samatta Amesajiliwa Fenerbahce

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania na aliyekuwa mchezaji wa Aston Villa – Mbwana Samatta, sasa ni rasmi amekamilisha usajili wa kuichezea Fenerbahce ya Uturuki msimu huu. 

Samatta alisajiliwa na Aston Villa mwezi Januari akitokea Genk – Ubelgiji. Akiwa Aston Villa amecheza michezo 16 na kuzifumania nyavu mara 2 pekee. Alitua Villa kwa ada ya pauni milioni 10 na alisaini mkataba wa miaka 4 na nusu.

Baada ya kutokuwa na mwanzo mzuri kwenye EPL akiwa na Villa, sasa amesajiliwa Fenerbahce na anakwenda kukipiga katika ligi ya Uturuki. Kwa sasa tayari Villa wameshasajili washambuliaji wawili akiwemo Ollie Watkins na Bertrand Traore.

“Ninajua Fenerbahce ni klabu kubwa. Ninafurahi kuwa kwenye familia hii, itakuwa ni changamoto mpya na kubwa kwangu.

Fenerbahce inamashabiki wengi na wanahitaji ushindi kila mara. Na mimi ninataka kushinda, nimekuja hapa kwa sababu hiyo. Nimefurahi sana na ninaimani tutashinda makombe mengi.” amesema Mbwana Samatta.


FURAHIA KASINO YA MTANDAONI

Tembelea ardhi ya maajabu ushangazwe na mengi ikiwa ni pamoja na urahisi wa kujipatia utajiri kupitia Kasino ya Meridianbet.

Cheza Sasa

41 Komentara

    Sio mbaya endelea kupambana

    Jibu

    Ni hatua nzuri ya mbwana samata kuchezea timu ya fenerbahce kila la kher

    Jibu

    Endelea kupambana bwana mkumbwa

    Jibu

    Endelea hadi kieleweke

    Jibu

    kila la kheri samatta kaoneshe maajabu zaidi ata waliokudharau wakuheshimu mwisho wa siku

    Jibu

    Kazi nzuri pongezi kwako endelea kupeperusha bendera ya,watanzania!!

    Jibu

    Hongera sana samatta kazi nzuri unayofanya ndio inakufikisha ulipo

    Jibu

    Lets go our Captain, Sam Magoli, Ulipo tupo, Fenerbahce new deal in Tanzania

    Jibu

    Kila la khery huko uwendako endelea kukiwasha mashabiki tupo nyuma yako

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Fenerbahce wamelamba dume

    Jibu

    Safii Sana kila La Kheri Sam kwenye makazi yako utayo salia kipige kokote kambi

    Jibu

    Samatta amepata dili nono kapambane kijana upeperushe bendera ya Tanzania

    Jibu

    Samata inabid apambane huko arud kwenye hadh yake

    Jibu

    Kila la kheri kaka huko aendako naona hadhi yako inazidi kupanda

    Jibu

    Pongezi kwake zidi juhudi na maharif uzid songa mbele zaid!!

    Jibu

    All in all kapambane tu

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Kilalakheri jembe

    Jibu

    Kila la kheri

    Jibu

    Atafika tu alipokusudia. Hatua kwa hatua

    Jibu

    hatua nzuri ya mbwana samata kuchezea timu ya fenerbahce Kila la kheri

    Jibu

    Sio mbaya Fenerbahce ni timu kubwa.keep it up

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Samatta hanazidi kuipeperusha bendela ya Tanzania kila la kheri ulipo nasisi tupo

    Jibu

    Asipoongeza jitihada ndio mwisho wake wa kuruka ruka huo

    Jibu

    Hongera sana katika timu hiyo ninaimani utapata nafasi nyingi kama utajitema vema mana huko hakuna ubaguzi kwa sababu timu imetawaliwa na wachezaji black

    Jibu

    Tunakunakutakia maisha mema

    Jibu

    Yote sawa piga kazi jembe

    Jibu

    Si sawa tu hata huko alipoenda kikubwa kuongeza juhudii tu

    Jibu

    Daah ila kila hatua dua kila la kheri samatha

    Jibu

    Good news

    Jibu

    safi samata sisi tunakuombea uzidi kufanya mazuri

    Jibu

    Jambbo la kheri

    Jibu

    Atafunga sana hapo

    Jibu

    Deal done , Safi Sana samatta endeleza mapambano.

    Jibu

    Kila la kheri kaka huko aendako naona hadhi yako inazidi kupanda

    Jibu

    Ulipo tupo

    Jibu

    Samatta kila la kheri

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.