Sureboy Kwasasa Hutuhusu, Hadi Uje Kariakoo

Baada ya kazi kubwa sana na tafiti ya muda mrefu, Gregor Mendel alifanikiwa kugundua mahusiano yaliyopo kati ya Jeni(Gene), urithi na tabia baina ya uzao na uzao. Hapo kabla dunia haikuelewa haya mambo.
.
Mendel aliwasilisha tafiti zake kwa wanasayansi wenzake ili wapate kutambua alichokifanya. Kwa bahati mbaya hawakumuelewa, wakazikataa tafiti zake kwa madai kuwa wanazifanya uchunguzi zaidi. Walitoa majibu ya kukubali alichokifanya miaka 16 baada ya Mendel kufariki. Huzuni iliyoje! Mendel hakuwahi kuona matunda ya kazi yake duniani.
.
Baada ya mapigano na mapambano ya damu na jasho Afrika Kusini wakafanikiwa kuimaliza sera ya ubaguzi wa ‘apartheid’ 1994. Hakuna asiyelitambua jina la Nelson Mandela nyuma ya mapigano yale. Walter Sissulu na Oliver Tambo ni kati ya wachache wengine wanaokumbukwa.
.
Ila vipi kuhusu Lalao Chiba alioandaa mipango na mikakati yote ya Mandela? Vipi kuhusu miaka 18 aliyosota kwenye chumba cha baridi jela? Nani analikumbuka jasho la Lonny Nkosi na David Webster? Vipi kuhusu uhai wa Steve Biko? Tunaikumbuka tu miaka 27 ya Mandela jela.
.
Najua na mimi nazingua ndiyo maana nimemchelewesha Sureboy hivi. Hizo stori za akina Mandela zinahusu nini? Najua hata mimi sipo ‘fair’ ndiyo maana nitamzungumzia Sureboy kwa sentensi kadhaa tu. Mbona hao akina Clatous Chama na Haruna Niyonzima nawaandikia maneno mtaa mzima?
.
Ila kweli haya maisha tumemchagulia Sureboy kwasababu tu hachezi Kariakoo? Licha ya ufundi wote alionao, HATUJALI. Sisi tunawahusudu waliovaa jezi zetu. Watanzania wengine hawatuhusu. Sisi tunajali kuhusu pasi za Fei Toto tu, sisi tunajali kuhusu ufundi wa Ibrahim Ajib tu. Sureboy hatuhusu. Si wetu huyu. Au tunasubiri apite kama Mendel ndo tumtambue? Au tumemchagulia historia ya akina Steve Biko?


Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!

Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!

Soma Zaidi

23 Komentara

    Sure boy mchezaji makin azam imepata mtu

    Jibu

    Wana kkoo tunamsubir kwa hamu kwny mitaa ya Twiga na jangwan pale

    Jibu

    Akienda jangwani ndio dunia itamuelewa

    Jibu

    Sure boy matata jangwan ni kwako

    Jibu

    Sure boy utakapo nenda tu

    Jibu

    Sure boy namkubali sana ila akija jangwani itapendeza

    Jibu

    sure boy anajua mpira uyu jamaa msimbazi akitua itakuwa ni jambo jema ila yeye ndo muamuzi ni wapi aende

    Jibu

    Kama sure boy anataka kuja mitaa ya kkoo tunamsubilia kwa hamu sana

    Jibu

    Itakuwa bora zaidi akienda Jangwani

    Jibu

    Karibu jangwani

    Jibu

    Kifupi Sureboy hana Nyota lakini shughuli yake dimbani ni Pevu sana, Huenda umakini na kulewa sifa mapema ndio kumempoteza mapema midomoni mwa watu. Sidhani kama muda unaruhusu kwa Sure Boy kujiuliza kwa mara ya pili au afanye tuu kama anakamilisha historia yake ya Soka.

    Jibu

    Sure abaki kwenye timu yake..jangwani itakupotezea mda tu

    Jibu

    Sureboy yeye mwenye maamuzi yake atakuwa chakufanya

    Jibu

    Sureboy yeye mwenye maamuzi yake atakuwa chakufanya

    Jibu

    Sureboy mtu hatari lkn hawiki kama wezake

    Jibu

    Sureboy ni nomaaa

    Jibu

    sure boy njoo zako jangwani

    Jibu

    Ukweli tu sure boy yupo vizuri ila ndio ivyo tena hana nyota

    Jibu

    Sure boy mchezaji mzur tatzo mfupi Sana doh.

    Jibu

    Sure boy yupo vizuri

    Jibu

    jangwani ndio dunia itamuelewa

    Jibu

    Kifupi Sureboy hana Nyota lakini shughuli yake dimbani ni Pevu sana, Huenda umakini na kulewa sifa mapema ndio kumempoteza mapema midomoni mwa watu. Sidhani kama muda unaruhusu kwa Sure Boy kujiuliza kwa mara ya pili au afanye tuu kama anakamilisha historia yake ya Soka.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.