Pogba Bado Anandoto ya Real Madrid

Kiungo wa Man United na timu ya Taifa ya Ufaransa – Paul Pogba, bado anandoto ya kuitumikia Real Madrid akiwa kama mchezaji.

Pogba amekuwa akihusishwa sana na Real Madrid haswa baada ya Zinedine Zidane kutamka hadharani hamu yake ya kumuona Paul akitumikia kikosi anachokifundisha.

Maisha yake ya soka yalianzia Man United ambapo alipata umaarufu akiwa bado ni kijana mdogo na baadaye aliuzwa na kujiunga na Juventus.

Akiwa Juve alifanya mambo mengi mazuri akitengeneza safu nzuri ya kiungo na Andre Pirlo ambaye kwa sasa ni kocha wa timu hiyo.

2016 Pogba alisajiliwa tena Man United akiwa katika kiwango cha juu sana. Maisha yake ndani ya United yamekuwa ni ya kupanda na kushuka, msimu baada ya msimu, kiwango chake hakitabiriki na wengi wanahisi bado hajaonesha uwezo ule aliotoka nao Juventus.

Akiwa amebakiwa na mwaka 1 kwenye mkataba wake, pengine wengi tulidhani angesajiliwa na timu kubwa katika dirisha hili la usajili ambapo bado hajaongezwa mkataba mpya na Man United, hali haikuwa hivyo na mpaka sasa ni mchezaji halali wa Man United.

Akizungumza na waandishi wa habari akiwa Ufaransa, Pogba amesema “kila mchezaji angependa kucheza Real Madrid. Ni ndoto yangu, sasa kwanini isitokee siku moja?

“Nipo Manchester na ninaipenda klabu yangu. Ninaichezea Manchester na ninafurahi, ninataka kufanya kila ninaloweza kuirudisha klabu mahali inapotakiwa kuwa. Nitajitoa kwa kila niliwezalo kama ilivyo kwa wachezaji wengine.”

Je, ndoto ya Pogba itatimia? Kuna mengi ya kuendelea kufurahia katika ulimwengu wa soka na hili ni moja wapo.


Weka Pesa kwa Airtel Money!

Sasa unaweza kuweka pesa moja kwa moja kwenye akunti yako ya Meridianbet kwa kutumia mtandao wa Airtel. Usipate wasi wasi, tunaifanya kazi kuwa rahisi zaidi!

Soma Zaidi

35 Komentara

    Pogba anawatishia tu man utd wamuongezee mshahara mnono

    Jibu

    Kambi popote kikubwa maslahi

    Jibu

    Pogba anataka kuwatia jambajamba united

    Jibu

    Pogba mtu mbad

    Jibu

    anaota

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Inapendeza sana

    Jibu

    Pogba kuenda madrid imekua stor alikua kwenye rada zao lakin sasa hawana uhitaj nae perez anaona hana umuhim wa kupoteza pesa

    Jibu

    Haend tu naona maisha ya United wamefika tamati kwake

    Jibu

    Ukitaka nenda tu kaka

    Jibu

    Pogba kuenda madrid imekua stor alikua kwenye rada zao lakin sasa hawana uhitaj nae perez anaona hana umuhim wa kupoteza pesa

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Kikubwa maslai kambi popote

    Jibu

    Uwezekano upo mkubwa sana kwa Pogba kutua Madrid

    Jibu

    Vizuri zitatimia tuu Pogba kilakitu kinakwenda namipango

    Jibu

    Ana mawazo manzur

    Jibu

    🔥

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Ni namna ya kujipigia debe ili asajiriwe na wakala wake mpende fedha anafurahia hilo kutokea. Nadhani angeweka akili yake Man U bila kuonyesha hisia zake kwamba angependa kucheza Real Madrid#meridianbettz

    Jibu

    Pogba akitua Real Madrid itakuwa vizuri naona Man u awana jipya

    Jibu

    Itakua poa sana akitua madrid

    Jibu

    safi tu

    Jibu

    Pogba nae akae atulie afanye maajabu asiwe mtu mwenye mawenge mara huku mara kule

    Jibu

    Safi tu

    Jibu

    Paul pogba anamsim mzur pale United pengne akiondok atuludsh makali

    Jibu

    Pogba yupo vizuri sana hakuna clabu ambayo hitakataa kumsajiri yeye tu apiganie hatimize ndoto zake

    Jibu

    Vizuri

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Good news

    Jibu

    Afanye kweli atimize ndoto

    Jibu

    maisha ya United wamefika tamati kwake

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Huenda ikawa kwel

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.