Kila mtu aliamini AC Milan wanaenda kutwaa ndoo yao ya saba. Hakuna aliyekuwa na shaka na hilo. Ilikuwa timu tishio sana duniani kwa wakati huo chini ya muitaliano Carlo Ancelotti.
Maajabu pekee ya dunia ni mashabiki wa Liverpool waliosafiri umbali mrefu hadi kufika Istanbul. Kila mtu duniani anawashangaa “wanaenda kufanya nini hawa mbele ya Rossoneri?”
Uwatazamapo Milan wana ukuta wa Allesandro Nesta na pacha wake Paolo Maldini. Usimsahau Cafu na Jaap Stam. Kikosini yupo Ricardo Kaka, Andrea Pirlo, Andriy Shevchenko pamoja na Gennaro Gattuso. Ilikuwa timu tishio sana!
![]()
Msimu ule Liverpool wamemaliza ligi kwenye nafasi ya tano, Waliwavuka Bayern Lervekusen, Juventus na Chelsea kama koni kwenye hatua za mtoano. Kwa upande wao Milan walitoka kuwaondoa Manchester United, Inter Milan na PSV Eindenhoven kisha wakapiga hodi kibabe fainali ya ligi mabingwa Ulaya.
Usiku ule jiji la Istanbul lilikuwa na nyuzi joto 18, ukungu wa asilimia 78 na upepo wa kawaida. Katikati anasimama refa kutoka Hispania Manuel Majuto Gonzalez kutafsiri sheria 17 za soka.
Bundi alianza kulia golini kwa Liverpool mapema tu dakika ya kwanza. Kitasa Paolo Maldini akawatanguliza Milan kwa krosi nzuri ya Andrea Pirlo. Maldini akaweka rekodi ya kuwa mfungaji mkongwe zaidi katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya.
Dakika ya 31, fundi mmoja wa ki-Argentina Herman Crespo anaweka mpira miguuni kwa Pirlo, Pirlo anaweka gozi kwa Maestro Kaka, kwa haraka Kaka anaonana na Shevchenko, kwa akili kubwa Sheva anaweka mpira kwenye njia ya Crespo. Ngoma kati, walete!

Dakika ya 44 ni yule mtu mbaya Ricardo Kaka, anakimbia chini kwenye counter kisha anaonana na Crespo ambaye anaweka tena kambini. Mashabiki wa Liverpool wanashika vichwa, kila mtu anaamini imeisha. Wanaenda mapumziko Liverpool wapo nyuma mabao matatu kwa sifuri.
ITAENDELEA..
Naam, hapa ni mahali pako! Kuwa shujaa kwenye sloti hii ya Samurai Ken ujishindie mkwanja na kujipa burudani murua.



Issa
Hii ndio anfield
Ernest
Wanabahatisha sana Liverpool
Amiri Kayera
Ilikua mechi kalii
Juliana Alex
Watakaa sawa tu
Ester mmakasa
Asante kwa kutujuza meridianbet.
aisha
Watakua sawa tuu
Dorophina
Liverpool msimu huu wanataka kupoteza mechi nyingi kizembe
Caroline
Liverpool wanajitaidi sana
Mwajumah
Watakua sawa tu
Adelta
Liverpool bado hawakosiriaz
Angelina
Liverpool miyeyusho
Fatina mfigi
Liverpool wajipange vizur
magdalena
liverpool wanaishi kwa mazoea
Sauda
Mechi ilikuwa ngumu sana
Nasra
Hi ndio Liverpool imekua moto toka ujio wa kloop
zeiyana
liverpool ya sasa hishapoteza muelekeo matokeo hayaeleweki
Janeflora malisa
Asnt kwa taarif
Fatuma kasomo
Wanabahatisha sana
Saupha mohamed
Liverpool IPO vizuri
Sabrina
Ilikua hatarii
Povel
Never walk a lone,This is Liverpool 🐓🐓🐓🐓🐓🐓🐓
Gabriel
Liverpool wajipange
Hidaya
Sio poa
felister
ilikua mechi kali
Lydia Emmanuel Magoti
Hiyo ndio Liverpool wazee wakukamia
Tatu
Mechi kali
Hopemwaikuka
🙈