KINARA wa pasi za mwisho kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu na nyota wa klabu ya Simba, Luis Miquissone βKonde Boyβ amesema kuwa amejipanga kufanya makubwa zaidi msimu huu wa 2020/21.

Akiwa amecheza mechi nne ndani ya Simba Luis amekuwa ni mtambo wa kutengeneza na kufunga mabao.
Luis amekuwa moto wa kuotea mbali msimu huu ambapo amehusika kwenye mabao sita kati ya 14 ambayo Simba imefunga kwenye michezo yao mitano iliyopita.

Amefunga bao moja na kutoa pasi tano za mabao na mchezo wake dhidi ya Biashara United wakati Simba ikishinda mabao 4-0 alitoa jumla ya pasi tatu rekodi ambayo bado haijavunjwa.
Akizungumzia kiwango chake Luis alisema: βNamshukuru Mungu kwa kuwa na mwanzo mzuri msimu huu, ambapo kwenye michezo mitano iliyopita nimefanikiwa kufunga bao moja na kuasisti mara tano, kwangu nimekuwa nikisema mara zote kuwa natamani kufanya vizuri kwenye kila mchezo kwa ajili ya mafanikio ya Simba.

βKiwango nilichofanikiwa kukionyesha kwenye michezo iliyopita na ushindani wa namba uliopo kwenye kikosi vimezidi kunipa ari ya kutaka kufanya vizuri zaidi, hivyo naamini nitakuwa moto zaidi kwenye michezo ijayo baada ya mapumziko ya kupisha michezo ya kimataifa kumalizika,β alisema kiungo huyo raia wa Msumbiji.
Naam, hapa ni mahali pako! Kuwa shujaa kwenye sloti hii ya Samurai Ken ujishindie mkwanja na kujipa burudani murua.Β



Issa
Miquison hafai sana
Ernest
Kama ni mpenzi wa soka kweli huwezi mkupinga uwezo wa Luis Miquissone, Ngoja tuone
Amiri Kayera
Anajua sana mpila af mpambanaji
Juliana Alex
Anajua
Ester mmakasa
Anajiamini sana kijana inapendeza.
aisha
Safi sana namkubali
Dorophina
Luis anauwezo mzuri wa kutoa pasi golini na mwengine akasababisha
Caroline
Hao ndo simba.
Mwajumah
Ni mpambanaji harafu anajua sana mpira
Adelta
Anajuwa Sana mpira halafu yeye ni mpambanaji mzuri uwanjani
Angelina
Yuko vizuri
Fatina mfigi
Kijan yuko vizur
magdalena
simba wanajiamini sana wamejipanga vya kutosha sana
Sauda
Anajitahidi kwa kweli
Shani
Ni mapambanaji
Nasra
Simba imepata mtu hapa
Janeflora malisa
Asnt kwa taarif
Fatuma kasomo
Gud news
Saupha mohamed
Simba IPO vizuri
Sabrina
Mi nasubiri nione alivyojipanga msimu huu
Povel
Luis mzee wa kuwa kera To be Continues ππΌππΌππΌππΌ
Gabriel
yuko vizur
felister
anajua sana mpira alafu mpambanaji
Lydia Emmanuel Magoti
Huyo ndio mmakonde alie chanjiwa kuja kukimbia uwanjani motowakuotea mbali huyo mbona watajiuliza juu yake
Tatu
Kijana yupo vizuri
Mwanahamisi
Kijana ni mpambanaji
Hopemwaikuka
Nmemuelewa