Mesut Ozil HAONDOKI!!!

Waswahili husema ‘ukimwaga mboga, namwaga ugali’. Mtanange wa Mesut Ozil na uongozi wa Arsenal bado mbichi!!!!!!!!!!

Pengine wengi tulitegemea Ozil ataondoka Arsenal baada ya kutojumuishwa kwenye kikosi cha timu hiyo msimu huu.

Timu nyingi zinatajwa kuiwinda saini ya kiungo huyu ambaye amekuwa na maisha magumu chini ya Arteta tangu mwishoni mwa msimu uliopita. Licha ya kuwa ndiye mchezaji anayelipwa pesa ndefu klabuni hapo, Mesut Ozil hatoitumikia Arsenal kwenye mchezo wowote msimu huu.

Siku si nyingi dirisha dogo la usajili litafunguliwa na pengine Ozil angeweza kuondoka. Kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyu, Ozil hatoondoka Arsenal mpaka mkataba wake utakapoisha mwishoni mwa msimu huu.

Inafurahisha lakini pia inahuzunisha kumuona mchezaji kama Ozil ambaye anauwezo na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Arsenal akiwa hatumiki huku timu hiyo ikitaabika kwenye EPL kwa kukosa wachezaji kama yeye.

Enzi za Ozil katika ubora wake ndani ya Arsenal.

Arsenal wanakwama wapi? 

Akizungumzia usajili wa Ozil, wakala wake – Dr Erkut Sogut amesisitiza ” Hata siku moja ni kubwa sana kwenye soka, huwezi kujua. Ni kweli, kunatimu nyingi zinazomuhitaji.

“Hii haijawahi kubadilika lakini pia utayari wake wa kuutumikia mkataba wake mpaka mwisho ni kitu ambacho hakijabadilika. Anayaishi maneno yake, ni muaminifu,  siku hizi ni vigumu sana kuupata uaminifu.

“Hafikirii klabu nyingine zaidi ya ambayo anamkataba nayo kwa sasa. Ni aibu Ozil hachezi, ni kweli kila mtu anautizama mshahara wake na ninaelewa ni kwanini. Kwa maono yangu, ninaona ni upotezaji wa muda ukizingatia kipaji na uwezo wake.

Ozil wa sasa akiwa na Arsenal.

“Nilizungumza na Arsenal siku chache kabla ya usajili na niliwaeleza hisia za Mesut, malengo yake ya kuendelea kubaki hapa na kiasi gani anaipenda klabu hii. Lakini hawakuwahi kuniambia kama hatokuwepo kwenye orodha ya wachezaji wao.

“Ilitushangaza sisi sote na ni kitu ambacho kilimuumiza sana Ozil.”

Unadhani kati ya Mesut Ozil na Arsenal, nani anayepata faida na nani anayeumia zaidi? Je, ni nini kifanyike kwa manufaa ya pande zote mbili?


BURUDIKA NA WANYAMAPORI WAKIIMBA NA KUPIGA VYOMBO VYA MUZIKI!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, furahia mchezo wa Forest Rock. Hapa utaburudika na umahiri wa wanyapori wanaoimba na kutumia vifaa vya muziki wa rock. Burudika huku ukijiwekea nafasi ya kutengeneza pesa ndefu kupitia Meridianbet!!

INGIA MCHEZONI!

19 Komentara

    Asiondoke ozili

    Jibu

    Arsenal mnazingua

    Jibu

    Arsenal hawaeleweki

    Jibu

    Ozil aende wapi sasa

    Jibu

    Ozili aondoke tu

    Jibu

    Ozili namkubali sana

    Jibu

    Safi sanaaa

    Jibu

    Yaan nyie arsenal hata siwaelew

    Jibu

    Arsenal wasikubali kumuachia ozil hata mkataba wake ukiisha

    Jibu

    Ozil hana chake

    Jibu

    Arsnal amsomekii

    Jibu

    Yuko vizuri

    Jibu

    Yupo vzr

    Jibu

    Safii Sana Ozil akibaki kusalia apo

    Jibu

    Arsenal nao waache ubabaifu sasa kuna faida gani kukaa na mchezaji wanamlipa ela ndefu na achezi wakumbuke Ozil anamashabiki wanaohitaji kumuona akicheza

    Jibu

    safi ozil

    Jibu

    Arsenal wanakwama wapi

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Bora wangemwacha aondoke mana wanamchanganya

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.