Dana Frederick White Linaweza kua jina Geni maskioni mwako lakini kwa taarifa yako huyu ndio njemba ambae anasimamia mapambano makubwa ya masumbwi ya uringo wa nyavu maarufu kama UFC yaani Ultimate Fighting Championship. Dana ndie anafanya UFC leo inaongeza wafuatiliaji kila kukicha kwakua ndani ya usimamizi wake kwenye mchezo huo tumemjua Conor McGregor, Khabib Nurmagomedov, Israel Adesanya na wengine wengi sana kwenye michuano ya UFC.

Dana White alizaliwa Julai 28 mwaka 1969 katika mji mdogo sana wa Manchester Connecticut ulioko wilaya ya Hartford huko nchini Marekani , Mwamba huyu ndio maana halisi ya biashara kwakua tangu yeye awe Raisi wa UFC taasisi hiyo imekua kimapato kiasi cha kupelekea utajiri wa bwana Dana White kufikia Dola za kimarekani milioni mia tano 500 USD ilipofikia mwezi Agosti mwaka 2019
Akiwa na umri wa miaka 17 tu alianza mchezo wa masumbwi baada ya kumaliza elimu yake ya sekondari katika shule ya Hermon High School huko Maine mwaka 1987 na kisha kujiunga na chuo mara mbili ya kwanza ikiwa ni Quincy College na ya pili ikiwa niUmass Boston na mwara zote aliacha muula wa kwanza .
Wanasema ndoto ni kuifukuzia bila kukata tamaa hili linajieleza wazi kwa Dana White kwakua licha ya kupambania masumbwi na kuto kufanikiwa alibaki na fani hiyo kama kocha na baadae Maimamizi wa baadhi ya wana masumbwi wakubwa Marekani.
Akiwa kama msimamizi wa Tito Ortiz na Chuck Liddell, Dana akakutana na Bob Meyrowits ambae alikua ni mmiliki wa Semaphole Entertainment Group ambayo ndio ilikua kampuni mama ya UFC. Dana alipogundua Bob Meyrowits anataka kuiuza UFC na yeye hakua na pesa ya kutosha kuimiliki alimtafuta rafiki yake wa utotoni bwana Lorenzo Fertita na kumshauri wainunue UFC.

Ilipofika mwezi Januari mwaka 2001 Lorenzo na mdogo wake Frank wakainunua UFC kwa Dola za Kimarekani Milioni Mbili na kumtangaza Dana White kua Raisi wa kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka 19 sasa na kupelekea kampuni hiyo kua na zaidi ya utajiri unaokadiriwa kufikia Dola za Kimarekani Bilioni 7 huku Dana White akimiliki asilimia 9 ya Kampuni hiyo.
BURUDIKA NA WANYAMAPORI WAKIIMBA NA KUPIGA VYOMBO VYA MUZIKI!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, furahia mchezo wa Forest Rock. Hapa utaburudika na umahiri wa wanyapori wanaoimba na kutumia vifaa vya muziki wa rock. Burudika huku ukijiwekea nafasi ya kutengeneza pesa ndefu kupitia Meridianbet!!



Shakila mrope
Asant san makala meridian bett
Mwanahamisi
Gud news
Adelta
Inapendeza
Caroline
Wanafanya vizuri.wafanye uwe ajira
neema hassan
Asante kwa taarifa@meridianbettz
samiah
Gud
Samira
Akiweka nia atafanikiwa kufikia lengo lake
warda
Dana anamawe kama yote