Kiungo wa kati wa Real Madrid Martin Odegaard hajajawa na msimu mzuri sana lakini sasa anajaribu kufanya jitihada kumshawishi bosi Zinedine Zidane.
Nyota huyu ambaye ni raia wa Norway amekuwa na changamoto, na amelazimika kuruka vizunzi kadhaa ili kuweza kuwa kwenye fomu nzuri na kukubalika na meneja Zidane.
Nyota huyu alipata jeraha ambalo lilimsumbua sana katika wiki za mwisho za msimu uliopita akiwa Real Sociedad kwa mkopo, msimu huu umeanza vibaya pia akipata changamoto ya jeraha kabla ya kujiweka vyema kwenye fomu.
Kurejea kwa Odegaard Madrid baada ya kutumikia kipindi chake cha mkopo kulianza kumpa matumaini kwa kurejeshwa kwenye kikosi cha kwanza.
Hata hivyo, hatma ya nyota huyu Real Madrid kwa miezi ijayo inategemea zaidi mchango wake katika nafasi yake ya kiungo klabuni hapo na katika matokeo ya klabu, lakini kwa sasa haiwezi kufahamika kama ni jukumu gani kubwa anaweza kulifanya.
Odegaard alipata wasaa wa kuanza katika michezo miwili ya kwanza ya msimu wa La Liga dhidi ya Real Sociedad na Betis kwa Madrid, lakini akapata majeraha ya misuli ikiwa ni sabababu iliyomfanya akose mechi sita na kisha nyingine tatu zaidi.
Nyota huyu wa miaka 22, sasa anaonekana kupona jeraha na anataka kuchukua jukumu kubwa kumshawishi Zidane na kuisaidia Madrid kusonga mbele. Wewe una mtazamo gani?
BURUDIKA NA WANYAMAPORI WAKIIMBA NA KUPIGA VYOMBO VYA MUZIKI!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, furahia mchezo wa Forest Rock. Hapa utaburudika na umahiri wa wanyapori wanaoimba na kutumia vifaa vya muziki wa rock. Burudika huku ukijiwekea nafasi ya kutengeneza pesa ndefu kupitia Meridianbet!!



Adelta
Hapo kazi ipo ajaribu lakini
Hopemwaikuka
Itakua poa sana
Rahma
Asante kwa makala
Dorophina
Nice update
Sarah
Du ajaribu aone kwanza
Janeflora malisa
Safi
Lydia Emmanuel Magoti
Duu kaz hipo hapo
Saupha mohamed
Jambo zuri
warda
Ajitahidi sana Zinade atamwelewa tu
Tatu
Jambo zuri