Ben Askren Akubali Kutinga Ulingoni na Mwana-Youtube Jake Paul. Jake Paul si mwanandondi haswaa, lakini ni mtu ambaye anajitengenezea umaarufu wake kupitia YouTube, amekuwa akisisitiza kuwa anataka kupanda ulingoni na moja ya mabingwa wa ndondi Conor Mcgregor.
Paul, ametoa ofa ya dola milioni 50 kwa Conor McGregor kukubali pambano na yeye, lakini McGregor hajaonesha kushobokea ofa yake.
Mwana-YouTube huyu amejaribu kuthibitisha uwepo wa fedha, au uhakika wa kitita kwa ajili ya pambano hilo lakini inaonekana kama ni kitu ambacho hakimshawishi McGregor ambaye kwa sasa amejikita zaidi kwenye maandalizi ya pambano lake la UFC 257 dhidi ya Dustin Poirier mapema Januari.

Hata hivyo, Ben Askren ameibuka na kusema kuwa angefurahi kuwa ulingoni na Jake Paul ambaye anaamini8 kuwa kwa kuwa si mwanandondi ameamua kuigiza kuwa yeye ni mwana michezo. Kwake itakuwa ni Burudani kuchapana naye ulingoni na kuchukua pesa kwa ajili ya pambano hilo.
Kwa upande wa McGregor, yeye anasema kama atarejea kutoka kustaafu kwake ndondi nasi atarejea kupambana na Manny Pacquiao. Hii inaonesha ofa kama ya Paul kwake si kitu anachokipa umuhimu.
Unadhani Jake Paul ni vyema akaanza na Ben Askren kabla ya McGregor?
VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???



Lydia Emmanuel Magoti
Pambano languvu hili
Adelta
Tunasubiri kwa ham Kuona pambano hilo nani ataibuka na ushindi
warda
Hadi raha
Shakila mrope
Mpambano wa kibabe
Rahmal
Mpambano wa ushindi
Ernest Kimeru
Ngoja tuone itakuaje
Saupha mohamed
Mambo moto
Issa
Hakutalalika
Hopemwaikuka
M nnavyopenda hela nngekubal tu
Sarah
Mambo nimoto