Kumekuwa na maneno mengi kuhusu sakata la Mo Salah kunyimwa unahodha kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa. Kocha – Jurgen Klopp alizungumzia hilo na kukiri kosa lake.
Katika mahojiano aliyoyafanya na kituo cha Diario AS, Salah alisema hadhani kukasirishwa na kitendo cha Klopp kumnyima unahodha kwenye mchezo dhidi ya Midtjylland na alienda mbali zaidi kwa kuzungumzia uwezekano wa kutimikia Real Madrid au Barcelona.
Kocha Jurgen Klopp ameona awekewazi kosa alilolifanya kwenye sakata hilo na amekiri kukosea kwake.

Jurgen amesema alizungumza na Salah kuhusu suala hilo na alifanya kosa kumpatia unahodha Trent Alexander-Arnold katika mchezo huo uliochezwa nchini Denmark.
“Nilikuwa nahodha kwa sehemu kubwa ya maisha yangu ya uchezaji, sijawahi kuona umuhimu wake. Hakuna cha ziada unachokipata sana sana ni kuwa na kazi kubwa tu.
“Sikuwahi na sioni umuhimu wa kuwa nahodha. Kabla ya mchezo (dhidi ya Midtjylland ) sikuona umuhimu wake kwa wachezaji, wala sikudhani kama ingekuwa ni stori kubwa kwa Trent.
“Hapa (Liverpool) tunasheria ya kuwa na kamati ya wachezaji. Kamati hiyo ni Jordan Henderson, James Milner, Virgil van Dijk na Gini Wijnaldum. Kimsingi hawa ndio manahodha wetu wanne.
“Kama wote hawachezi basi kikawaida mchezaji aliyekaa muda mrefu kwenye timu ndiye anakuwa nahodha. Ndivyo nilivyokuwa ninaitizama, na hapo ni Trent. Simaanishi kwenye safari yake ya uchezaji chipukizi, ninazungumzia kucheza kikosi cha kwanza.

“Baada ya hapo kunamtu aliniambia kwa kigezo hicho alipaswa kuwa Divok Origi, hivyo hilo ni kosa langu. Baada ya hapo nilizungumza na Mo Salah kuhusu hilo. Niligundua kwake haikuwa sawa na nilimueleza kila kitu kwa uwazi.
“Alifanya mahojiano kitu ambacho hakina shida yoyote kwangu. Ni kweli alikasirika . Sikufanya vile makusudi, na kama nilifanya kosa basi ilikuwa kutomkabidhi unahodha Divok Origi siku ile.” Alisema Klopp
Liverpool watakuwa uwanjani kupambana na West Brom Albion kesho katika dimba la Anfield.
VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???



warda
Bora Klopp ameona kosa lake ila Salaa mwenyewe haoni umuhimu wa unahodha ndo mana kamaind kidogo
Adelta
Klopp ni mtu anayejitambuwa ndiyo maana amekiri kosa
Rahmal
Klopp ni mtu muelewa sana na ndomana amekili
Sarah
Klopp nimtu anajielewa ndiomana ameona umuhimu wakukiri kosa lake
Lydia Emmanuel Magoti
Nikweli alifanya makosa
Ernest Kimeru
Ni wakati wa Klopp kuwa makini sasa
Latifa juma mohamed
Gud news.
Issa
Klopp asahihishe hili
Saupha mohamed
Klopp atulie sasa
Hopemwaikuka
Sawaa
Tatu
Klopp anajielewa sana