LeBron James, Durant na Middleton Wanang'aa NBA.

Usiku wa kuamkia leo, michezo kadhaa ya NBA 2020/21 imechezwa. LeBron James, Kevin Durant na Khris Middleton wanaendelea kung’ara msimu huu.

LeBron James ameendelea kufanya vizuri kwenye michezo yote aliyoicheza siku ya Krismasi. Mchezo dhidi ya Dallas Mavericks, James aliutumia kupanda nafasi na kuwa mchezaji wa 2 (nyuma ya Kobe Bryant) aliyefunga pointi nyingi zaidi kwenye michezo iliyochezwa Krismasi.

LeBron James (kulia)

LA Lakers waliibuka washindi kwa pointi 138-115 dhidi ya Mavericks. James alipachika pointi 22, alitoa pasi 10 za magoli na alicheza mipira 7 iliyokufa. Kwa takwimu hizi, LeBron James amefikisha pointi 383 akimzidi Robertson (377) na ni Kobe Bryant (395) pekee aliyemzidi James.

Kevin Durant ameendelea kufanya vizuri kwa kuisaidia Brooklyn Nets kuwaburuza Boston Celtics katika ushindi wa pointi 123-95.

Kevin Durant na Kyrie Irving (kulia).

Durant alipachika pointi 29 wakati ambapo mchezaji mwenzake Kyrie Irving alifunga pointi 37, alitoa pasi 8 za magoli na alicheza mipira 6 iliyokufa. Takwimu za Irving kwenye mchezo huo zimempandisha na anakuwa kwenye rekodi ya wachezaji waliofunga mipira ya pointi 3 (three pointer) mara 7 kwenye mchezo uliochezwa siku ya Krismasi.

Khris Middleton alikuwa shujaa wa Milwaukee Bucks katika mchezo dhidi ya Golden State Warriors.

Khris Middleton (kushoto) akipambana na Stephen Curry (kulia).

Middleton alipachika pointi 35, alitoa pasi 5 za magoli na alicheza mipira 4 iliyokufa katika mchezo ambao Bucks walishinda kwa pointi 138-99 na kuwaacha Warriors wakilala chali kwa mechi 2 mfululizo kwenye NBA msimu huu.


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini???

SOMA ZAIDI

13 Komentara

    NBA kwa sasa wako vizuri

    Jibu

    Hongera yao James anajitahidi sana

    Jibu

    Pongez sana kwao

    Jibu

    Hongera yake

    Jibu

    Ongera yao

    Jibu

    Hongera yao

    Jibu

    Kazi kazi

    Jibu

    Hongera yao

    Jibu

    Hongera zao

    Jibu

    Wazee wa nba

    Jibu

    Hongera yake

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Hongera yao

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.