Alikaa chini kwa tafakuri baada ya Mwandishi kumpiga swali moja gumu kidogo nguli wa habari Argentina bwana Daniel Arcos, alipoulizwa nini kitu muhimu zaidi maishani mwako na kinakufanya upende maisha?
Daniel akasema kwa Dear Gambe inanisafirisha kimawazo, pili wanawake ni tiba stress zinakufa, tatu pesa ambayo inaweza kuhamisha milima ya Olympus kutoka Ugiriki mpaka Ulanga Morogoro na nne ni Lionel Messi, mtoto mmoja anaecheza na kuwafundisha wenzie soka.

Alimaliza vipaumbele vyake Daniel na kumwambia Mwandishi bwana achana na mimi nipate gambe nyingine, Mwandishi nae akafunga dodoso lake na kuanza safari ya kurejea ofisini kwenda kujaza taarifa yake vyema, japo alistaajabu sana majibu ya Daniel ila alichoka baada ya kusikia ya Sergio Fernandes.
Sergio Fernandes ni msomi wa daraja la juu kwenye sheria nchini Argentina, ni moja kati ya Mahakimu wakubwa nchini humo nyuma ya sifa yake kubwa nchini mwake yeye aliweka nadhiri yake kuwa jezi aliyoinunua ya Diego Maradona wakati anatambulishwa Newell’s Old Boys 1993, atampa mrithi wake sahihi.

Zilipita siku, wiki, mwezi na hatimae miaka jezi namba 10 ya Diego Maradona inaoeza kabatini, mkewe Cathrine alimuuliza hii jezi itakaa ndani mpaka lini?? Sergio alimjibu mpaka pale mrithi wa Maradona atakapopatikana nitamkabidhi jezi hii, baada ya hapo nipo tayari kufa nikiwa nimetimiza nadhiri yangu.
Hiyo ilikuwa 2005, kesho yake tu Lionel Messi anaanza kuonyesha maajabu Camp Nou, ikapita tena miaka mpaka 2014 tayari Lionel Messi kafanya kila kitu kwenye dunia, Fernandes alipotaka kumpa Jezi akapigwa konga na police akafeli kumpa jezi yake lakini bado hakukata tamaa.

Kumbuka Fernandes ni msomi mkubwa aliwahi kuwa Jaji Mkuu wa Argentina, lakini anahangaika ili tu ampe Messi jezi ya Maradona kwakuwa anaamini ni mrithi wake, ndoto ikatimia 2018 kwenye kombe la dunia kwa msaada wa Mwandishi Vero Brunatti, Messi akapewa jezi yake.

Lionel Messi hakuvaa jezi hiyo kwakuwa aliamini kama Maradona bado yuko hai basi Mfalme ni yeye, ila siku alipokufa Messi alivaa hiyo jezi Novemba 25,2020 ikiwa ni miaka miwili tangu apewe, akafunga bao na kuionyesha, pia akaiambia dunia yeye ndie MFALME MPYA.

VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini?



Shakila mrope
Safi san messi
Sania
Safi jembe
Magdalena
Messi tangu zamani hana mpinzani
Rahmal
Messi Yuko vizuli baba lao
Gabriel
Anastahil maana kiukwel anajituma sana
felister
anastahili
warda
Mie mfalme kwangu ni CR7
Adelta
Messi ameanza vizuri 2021
Angelina
Messi yuko vizuri
Dorophina
Messi jembe
Lydia Emmanuel Magoti
Namkubali messi
Issa
Mess anatisha
Rehema
Safi
Saupha mohamed
Messi mtu mbaya
Chiku
Mess jembe