Manchester City wanaripotiwa kuwa wamungana na Juventus kwenye mbio za kuiwania saini ya kiungo wa Sassuolo Manuel Locatelli kwa dau la €35m.
Nyota huyu ambaye ni zao la akademi ya soka ya vijana ya Milan amefikisha umri wa miaka 23 tu wiki iliyopita, na mpaka sasa tayari ameshacheza mechi 6 za timu ya taifa ya Italia.
Juventus hawakuweka siri juu ya adhma yao ya kumtaka Locatelli, ambaye amecheza jumla ya mechi 126 za Serie A mpaka sasa akiwa na magoli sita na pasi za mwisho tisa.

Sasa kwa mujibu wa Daily Mail, pia jicho la Man City wa Pep Guardiola limetua kwa staa kinda huyu. Wakala wake Stefano Castelnuovo alinukuliwa akisema;
“Tuna uhusiano mzuri sana na Sassuolo, klabu ina mipango mikubwa sana. Tutaona nini kitatokea, kama ofa nzuri ikija, itakuwa ni heri kwa kila mmoja kufikia makubaliano”
“Lakini wakati wote tutawashukuru Sassuolo. Atawashukuru Milan wakati wote pia lakini nadhani atakuwa anatafuta changamoto mpya, Italia au nje ya Italia. Ana ndoto ya kucheza Ligi ya Mabingwa, bila shaka yeye na Sassuolo watapata zawadi msimu wa joto.
Ndio, kwetu Mteja ni mfalme. Jiunge sasa na familia ya Meridianbet bila malipo yeyote na sisi tutakuzawadia bonasi ya shilingi 3,500 kama sehemu ya kukukaribisha kwenye familia hii BURE!!!. Unasubiri nini??



Shakila mrope
Vizuri san
Sania
Good
Sadick
Scout ya Man City ipo makini na hubaini wachezaji mahiri ktk klabu yao. Utakuwa uasjiri makini
Caroline
Locatteli ni mchezaji mzuri Sana
Rahmal
Safi
Dorophina
Locatelli ni bora haelekee city
Magdalena
Maamuzi ni yake
Saupha mohamed
Safi
felister
maamuzi anayo yeye
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri
Hopemwaikuka
Yuko vzur
Sarah
Safi
warda
Imekaa poa sana