FA Cup: Fernandes Awaondoa Liverpool.

Baada ya kugawana pointi kwenye mchezo wa EPL wikiendi iliyopita, Liverpool na Man United walikutana tena kwenye FA Cup jumapili hii.

Vikosi vya timu zote vilibadilika katika mchezo wa mzunguko wa 4 wa FA Cup ambapo ni kombe lenye heshima kubwa kwenye historia ya soka la Uingereza.

Liverpool ilimkosa nahodha wake Jordan Henderson huku Sadio Mane akianzia benchi. United walimpumzisha Bruno Fernandes huku Dean Henderson akichukua mikoba ya De Gea kulinda goli.

Man United vs Liverpool ni mchezo wenye upinzani mkali kwa miaka mingi. Licha ya Salah kuanza kutikisa nyavu za United dakika ya 18, Greenwood alisawazisha na Rashford akaongeza la pili. Muda mfupi baadae, Salah alisawazisha kabla ya Fernandes kuwapatia ushindi United kwa mpira wa faulo dakika ya 78.

Bruno Fernandes akipachika goli la ushindi kwa Manchester United.

Kipigo cha Liverpool kutoka kwa United kinaendeleza takwimu mbaya za Liverpool dhidi ya United katika uwanja wa Old Trafford, Liverpool wameshinda mchezo 1 kati ya 15 waliyocheza katika uwanja huo.

Kwa ujumla, Liverpool anakamilisha michezo 4 bila kupata ushindi katika mashindano yote. Msimu uliopita, Liverpool alitoka katika mzunguko wa 5 wa FA Cup lakini msimu huu, safari yao imeishia mzunguko wa 4.

United watachuana na West Ham United katika mchezo wa mzunguko wa 5 mwezi Februari, 2021.


MSHINDANI HUSHINDA BWANA!

Anayejaribu hawezi kutoka kapa Meridianbet! Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet inakuhakikishia ushindi mkubwa kila unapojaribu kuingia mchezoni. Washindi hushindana, ingia mchezoni!

Fairy-in-Wonderland_Casino-Post_25-January

CHEZA SASA

15 Komentara

    Fernandes alinikosha sana

    Jibu

    Good

    Jibu

    Jambo jema

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    United mlifanya kitu kizuri sana

    Jibu

    Good

    Jibu

    Safi san inapendeza

    Jibu

    Fernandes anaendela kujenga ufalme wake ndani ya Man U

    Jibu

    Fernandes alijua kutufurahisha mashabiki wa man u

    Jibu

    Nakubalii

    Jibu

    Fernandes mtu mbaya akoseagi

    Jibu

    Goodnews

    Jibu

    Good

    Jibu

    United inepata

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.