Kiungo wa PSG, Leandro Paredes ameweka wazi kuwa klabu yake ipo kwenye mchakato wa kutaka kumsajili nyota wa Barcelona Lionel Messi.
Messi, ambaye ana hostoria kubwa na klabu ya Barcelona, amekuwa akihusisishwa na kuondoka Camp Nou wakati mkataba wake pia ukiwa ukingoni. Mabingwa wa Legue 1, PSG na miamba ya EPL, Manchester City wote wamekuwa wakihusishwa na saini ya staa huyu.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa mbali mbali kufika kwa Pochettino pale PSG, kumeongeza uwezekano wa klabu hiyo kuiwinda saini ya Messi. Leandro Paredes anasema kuwa klabu yake inafanya jitihada za kuinasa saini ya nyota huyo anayemaliza mkataba wake mwisho wa msimu.

“Ni juu ya klabu, wanajaribu kumshawishi. Kuweza kufundishwa na kocha anayetokea nchini kwako na uwezekano wa kucheza na Messi ni fursa kubwa, natumaini itakamilika.” – Paredes
Ikiwa dili hili litakamilika, Messi atakuwa anakutana na msela wake aliyekuwa naye Barcelona, bwana Neymar.
Anayejaribu hawezi kutoka kapa Meridianbet! Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet inakuhakikishia ushindi mkubwa kila unapojaribu kuingia mchezoni. Washindi hushindana, ingia mchezoni!



warda
Itakuwa poa sana Messi akitua PSG hata mie nitakuwa shabiki wake
Venerose
Messi sense tu PSG
Adelta
Itapendeza Sana
Rahmal
Safi sana
Venerose
Messi aende tu PSG
Sania
Itakuwa vizuri akienda huko
Magdalena
Wajipange sana kumpata
Sarah
Watafanya Jambo zuri
Ernest Kimeru
PSG wanataka kumwaga mpunga tena
Dorophina
Itakuwa poa sana safari hii PSG wasiferi kumbeba messi
Mwanahamisi
Safi
Hopemwaikuka
Itakua vyema
Lydia Emmanuel Magoti
Itakuwa poa
Angelina
Itakuwa poa
Saupha mohamed
Safi
Issa
Mess bado psg