Hadithi ya Klopp na Tuchel

Hii ni simulizi ya kusisimua makocha wawili wa kijerumani wanaofundisha vilabu vya England; Jurgen Klopp wa Liverpool na Thomas Tuchel wa Chelsea.

KLOPP

Kabla ya kutua Liverpool alikuwa kocha wa Dortmund na taji lake la mwisho lilikuwa ngao ya jamii 2012. Alipoenda Liverpool 2015, mechi yake ya kwanza ikaisha kwa sare tasa ya 0-0. Kilichofuata baada ya hapo ni mataji mfululizo hadi Liverpool wakakosa pa kuyaweka.

TUCHEL

Kabla ya kutua Chelsea alikuwa kocha wa PSG na taji lake la mwisho ni ngao ya jamii. Alipoenda Chelsea, mechi yake ya kwanza imemalizika kwa sare tasa yaani 0-0.

Ni kwa mgongano huu wa matukio wataalamu wanaona kwamba Chelsea wajiandae kunyeshewa mvua ya mataji.

KWANINI?

Klopp na Tuchel ni watu wenye historia ndefu na ya kusisimua sana.

Klopp alikuwa kocha wa Mainz 05 ya Ujerumani hadi mwaka 2008 alipoondoka na kwenda Borussia Dortmund. Nafasi yake ikachukuliwa na Thomas Tuchel.

Alikaa Dortmund hadi 2015 alipoondoka na kuchukua mapumziko mafupi. Nafasi yake tena ikachukuliwa na Tuchel.

Utaona ni namna gani walivyokuwa wanafuatana kila wanakoenda, kwanini mataji pia yasiwafuate?

MAJINA YAO

Jina la Klopp linafanana na Kop, ambalo ni jukwaa la mashabiki lia lia wa Liverpool. Kop ni jina maarufu na ni kama moja ya alama za klabu hiyo.

Jina la Tuchel pia linafanana na Chelsea hasa katika kipindi hiki ambacho kulikuwa na tetesi za yeye kwenda darajani.

Tuchel inafanana na To Chelsea, sentesi iliyotumika kumhusisha na Chelsea na hata alipotangazwa rasmi kujiunga darajani.

NI HIVI

Kufanana kwa majina haya na vilabu vyao kunajenga muunganiko wao na vilabu, kama ilivyokuwa kwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger.

Unaikumbuka Arsenal ya Arsene?


MSHINDANI HUSHINDA BWANA!

Anayejaribu hawezi kutoka kapa Meridianbet! Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet inakuhakikishia ushindi mkubwa kila unapojaribu kuingia mchezoni. Washindi hushindana, ingia mchezoni!

Fairy-in-Wonderland_Casino-Post_25-January

CHEZA SASA

13 Komentara

    Simulizi inapendeza

    Jibu

    Urafiki ni Jambo jema

    Jibu

    Iko vizuri 👍

    Jibu

    Utafiki wao ulikuwa mzuri

    Jibu

    Klopp na Tuchel wote ni malegend

    Jibu

    Urafiki wao ulikuwa Safi sana

    Jibu

    Iko poa

    Jibu

    Sasa imekuwaje saiz urafiki unasaidia kusaidiana kwenye shida

    Jibu

    Iko poa snaa

    Jibu

    Mambo hayo

    Jibu

    Historia nzur sana

    Jibu

    Historia imetulia

    Jibu

    safi sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.