Simba: Bingwa wa Super Cup Kuchukua Milioni 15

Uongozoi wa Simba umeweka wazi kuwa zawadi atakazopata bingwa wa michuano ya Simba Super Cup iliyoanza Januari 27, 2021 ni fedha taslimu shilingi milioni 15, kikombe na medali.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wamepanga kutoa zawadi hiyo pamoja na kutoa burudani kwa mashabiki ambao watajitokeza kutazama mashindano hayo ambayo ni mara ya kwanza kufanyika ndani ya ardhi ya Bongo.

Katika mashindano hayo ni timu tatu ambazo zinashiriki ikiwa ni Simba wenyewe ambao ni wenyeji, Al Hilal ya Sudan na TP Mazembe ya Congo.

Simba ilianza mchezo wa ufunguzi Januari 27 na ilishinda mabao 4-1 dhidi ya Al Hilal na mchezo wa pili ulikuwa ni jana, Januari 29 ambapo Al Hilal ilishinda mabao 2-1 dhidi ya TP Mazembe.

Kilele ni kesho Januari 31 ambapo Simba itacheza na TP Mazembe na mshindi atapatikana kesho, Uwanja wa Mkapa.

Manara amesema baada ya mchezo wa mwisho kutakuwa na tafrija (after party) ambayo itafanyika ‘Kidimbwi Beach’ jijini Dar es Salaam.

Na siku hiyo kutakuwa msanii wa Bongo Fleva Zuchu ambaye katika mchezo wa mwisho wa michuano hiyo utakaopigwa Jumapili, Januari 31, 2021 kati ya Simba vs TP Mazembe atatoa burudani.

Manara amesema:”Tumejipanga na tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kushangilia na kuona burudani, pia atakuwepo Zuchu ambaye yeye mwenyewe amesema kuwa mchezaji anayemkubali ni Aishi Manula ila siyo kumzimia maana nyinyi hamuishiwi maneno.

“Ila hata kama akimzimia hakuna tatizo Manula anajulikana na ni miongoni mwa watu ambao huwa wanaandamwa wakifanya makosa licha ya kwamba ni kijana mtaratibu,”.


MSHINDANI HUSHINDA BWANA!

Anayejaribu hawezi kutoka kapa Meridianbet! Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet inakuhakikishia ushindi mkubwa kila unapojaribu kuingia mchezoni. Washindi hushindana, ingia mchezoni!

Fairy-in-Wonderland_Casino-Post_25-January

CHEZA SASA

12 Komentara

    Safi snaa simba

    Jibu

    Simba inapendeza Sana 👏👏

    Jibu

    Sawaaa.

    Jibu

    Simba ipo vizuri

    Jibu

    Simba juuuu

    Jibu

    Ngoja tuone ni Nani ataibuka na ushindi

    Jibu

    Simba iko juu

    Jibu

    Safiii Sana Simba pongezi zao

    Jibu

    Simba wako vzur

    Jibu

    Tunasubilia kuona nani ataibuka kidedea

    Jibu

    Simba baba lao hi

    Jibu

    Huyo haji sio kwa kuvimba huko

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.