Tetesi zinasema Liverpool wanapanga uhamisho wa mkopo kwa mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa New York Red Bulls Aaron Long, 28. Klabu hiyo ya Anfield inajiandaa kutumia saa 72 za mwisho za dirisha la usajili, kumsajili mlinzi wa kati baada ya Joel Matip kuwa majeruhi.
Tetesi zinasema Real Madrdid watatupa karata yao kwa mshambuliaji wa Ufaransa na Paris St-Germain Kylian Mbappe, 22, msimu huu.
Tetesi zinasema Paris St-Germain wana nia ya kuwaunganisha tena kocha Mauricio Pochettino na kiungo wa Tottenham Dele Alli, 24.

Tetesi zinasema winga wa England na klabu ya Leicester City , Demarai Gray, 24, ameridhia masharti binafsi na Bayer Leverkusen lakini klabu hizo mbili vinavutana kuhusu ada.
Mchezaji wa nafasi ya ulinzi Sergio Ramos, 34, bado hajakubali mkataba mpya na Real Madrid, mwezi mmoja baada ya pande hizo mbili kukutana kujadiliana kuhusu kuongeza mkataba wake, ambao utakwisha msimu huu.
Timu ya Uturuki ya Trabzonspor inaamini imefikia makubaliano ya kumsajili beki wa kushoto wa Tottenham Danny Rose, 30.
Tetesi zinasema Manchester City wanakaribia kuwasajili makinda mawili wa Fluminense na raia wa Brazil Kayky na Metinho, wote wenye umri wa miaka 17, kwa kitita cha pauni milioni 9.
Southampton na Westbrom wanajaribu kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal Ansley Maitlan-Niles,23, kwa mkopo kabla ya dirisha la usajili la mwezi Januari kufungwa Jumatatu.
Klabu hiyo ya Pep Guardiola haina mpango na mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Bayern Munich David Alaba, 28, kwa kuwa klabu inampango wa kumsajili mchezaji wa nafasi ya ushambuliaji.

Tetesi zinasema kocha wa zamani wa Chelsea na Tottenham Andre Villas-Boas, 43, anatarajiwa kuondoka Marseille mwishoni mwa msimu.
Mshambuliaji wa Wolves Patrick Cutrone, 23, anajiandaa kujiunga kwa mkopo na klabu ya Valencia kwa msimu wote uliosalia baada ya uhamisho wake kwa mkopo katika klabu ya Fiorentina kumalizika mapema.
West Brom wamekubali kumsajili kiungo wa kati wa Celta Vigo,Okay Yokuslu, 26, ingawa wanahitaji kumshawishi mchezaji huyo.
Tetesi zinasema mchezaji wa Aston Villa, Mfaransa Frederic Guilbert, 26, amekubali uhamisho wa mkopo kuelekea Strasbourg.
Tetesi zinasema Mshambuliaji wa Everton Cenk Tosun, 29, anataka kurejea kwenye klabu yake ya zamani ya Besiktas kwa mkopo.
Mlinda mlango wa Denmark Jonas Lossl,31, ataondoka Everton na kusajiliwa na klabu yake ya zamani ya FC Midtjylland.
Anayejaribu hawezi kutoka kapa Meridianbet! Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet inakuhakikishia ushindi mkubwa kila unapojaribu kuingia mchezoni. Washindi hushindana, ingia mchezoni!



Adelta
Tetesi zinasomeka
Caroline
Asante kwa taarifa
Sania
Tetesi zimetulia
Venerose
Makala imetulia
Khadija
Asante kwa taarifa
Magdalena
Naona dirisha dogo la usajili Mambo yanazidi kupamba Moto
Sarah
Tetesi safi
Lydia Emmanuel Magoti
Tetesi zipo poa
Dorophina
Liverpool watafanikiwa kumsajili mchezaji huyo kwa masaa yaliyobaki
Rahmal
Hasante meridian kwa makara nzuli
samiah
Safi