Sami Khedira ametuma ujumbe kwa mashabiki wa Juventus kwenye mitandao ya kijamii kuwa wakati wote atawaombea heri katika mafanikio yake. Mshindi huyu wa Kombe la Dunia akiwa na Ujerumani 2014 alijiunga na Hertha Berlin baada ya kumaliza kandarasi yake na Juventus.
“Kila safari ina mwisho. Lakini kumbukumbu zitabaki kila wakati, lilisomeka chapisho la nyota huyu miaka 33 kwenye ukurasa wake wa Instagram.”

Sehemu kubwa ya ujumbe;
“Mpendwa mwana Juventus,
“Ningependa kukushukuru kwa moyo wangu wote! Ilikuwa vyema sana katika wakati wote wa mafanikio. Kama timu, tumeshinda mataji matano ya Serie A kwa miaka mitano, tukishinda Coppa mara tatu na Kombe la Super mara moja. Ninajivunia kuwa sehemu ya wakati huo.”
“Kwangu imekuwa heshima daima kuvaa uzi huu wa kushinda tuzo na ninaondoka na kumbukumbu za wakati bora.”
“Watu wanaifanya timu hii kuwa maalum na ninafurahi sana kuwa nimekutana na sio wachezaji wenzangu tu, bali marafiki wa kweli. Nawatakia bahati nzuri kwa siku zijazo. ” – Sehemu ya ujumbe wa Khedira
Juventus pia wamechapisha katika tovuti yao ujumbe wa shukrani kwa nyota huyu. Khedira alikuwa sehemu muhimu ya Juventus licha ya ukweli kuwa hakuweza kupata nafasi ya kucheza mechi yeyote msimu huu.
Neptune’s Richies ni mchezo Unaokupa pesa chap chap huku ukiwa unaburudika kupitia Kasino ya Mtandaoni ndani ya Meridianbet.



Magdalena
Alilosema ni Jambo la kweli kabisa
Lydia Emmanuel Magoti
Yupo sahii kwa alicho kiongea
Sarah
Ni kweli kabisa kwa alichokiongea
Caroline
Kweli kabisa
Rahma
Yuko saihii kea alichokisema
Dorophina
Sami yuko sahihi kabisa
Hopemwaikuka
Ni sawa
Sania
Sami amesema kweli
Janeflora malisa
Asnt kwa taarif
Venerose
Asante kwa makala
warda
Ujumbe mzito sana