Yanga Afrika kuna dhoruba, imepiga Tsunami na nyumba za watu zimemezwa. Wananchi wakiwa hoi hawana hili wala lile, serikali ya taifa la Yanga Afrika inatafutana, ghafla walikuja msalaba mwekundu kuokoa maisha ya watu. Yanga Afrika ikapata tumaini jipya.
Yanga Afrika kuna njaa, wananchi wanateseka na serikali haijui itapata wapi chakula. Ghafla walikuja WFP kutoka kusikojulikana na kutoa chakula.
Yanga Afrika kuna mgomo, wafanyakazi hawajalipwa kwa miezi kadhaa na wamegoma kwenda kazini. Wakati serikali ya Yanga Afrika wanajiuliza wanawalipa vipi wafanyakazi wao, ghafla walikuja IMF na kuwarudisha kazini.
Yanga Afrika kuna ukata, nchi imeshindwa kuajiri na wanapigwa bao na nchi zingine, haswa hawa majirani zao wa Lunyasi. Serikali kichwa kinauma hawajui pesa inapatikana wapi, ghafla ilikuja benki ya dunia na kuajiri upya. Yanga Afrika ikapata wafanyakazi bora tena.

Yanga Afrika kuna gonjwa la mlipuko, linatishia uhai wa wananchi na hawana uhakika na afya zao. Serikali haina dawa na madaktari wa kutosha. Ghafla walikuja WHO na kusaidia utafiti, wakalipa wataalam na ugonjwa ukaondoka.
Yanga Afrika kuna uhaba wa miundombinu, barabara zimeharibika na usafiri umekuwa shida. Serikali wamekaa kimya na kujifanya hawaoni. Ghafla ulikuja msaada kutoka nchi ya ugeni. Wakarekebisha miundombinu na kazi zikafanyika kwa urahisi tena.
Yanga Afrika kuna sintofahamu, wananchi wameigomea serikali. Hawatokei kwenye vikao na shughuli zote za kiserikali. Wakati haya yanaendelea, waliletwa watu wa kutoa hamasa, na ghafla wananchi wakaanza kujaza viwanja kwenye shughuli zao kama zamani.
Yanga Afrika kuna vita, amani imepotea na nchi haina jeshi la kupambana, wananchi hawana uhakika na maisha yao. Ghafla walitokea UN na kutuma askari, wakapiga vita na amani ikarejea Yanga Afrika tena.
Nchi ya Yanga Afrika ni klabu, serikali ni uongozi wa hili taifa, Msalaba mwekundu, WHO, UN IMF na hao wengine wanaozungumza hapa ni GSM. Wametokea ghafla, na ghafla Yanga Afrika imetulia na kuna amani. Yanga Afrika wanaishi tena kama zamani. Kongole GSM.
Neptune’s Richies ni mchezo Unaokupa pesa chap chap huku ukiwa unaburudika kupitia Kasino ya Mtandaoni ndani ya Meridianbet.



Janeflora malisa
Asnt kwa taarif meridianbet
Magdalena
Kweli yanga walikuwa na kipindi kigumu lakini Sasa hivi mambo shwali
Rahma
Yanga asaivi wanazidi kuwa moto
Adelta
Kwa Sasa kidogo wanajitahidi
Caroline
Yanga kuna nn tena
Dorophina
Nice update
Venerose
Yanga wako vinzur
Sarah
Yanga kwasasa wako vizuri
Hopemwaikuka
Haya buana
Sania
Hongera wana Yanga
Lydia Emmanuel Magoti
Mambo hayo
warda
Wangekuwa matonya washkuru