China Wamtaka Michael Sarpong

Imefichuka rasmi kuwa klabu ya Yanga ipo tayari kumuachia mshambuliaji wao Michael Sarpong endapo tu kama kuna timu itakuwa tayari kulipa fedha kiasi cha shilingi bilioni 1.2 kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji huyo.

Sarpong mwenye uraia wa Ghana alijunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea katika klabu ya Rayon FC ya nchini Rwanda katika usajili wa dirisha kubwa, ambapo tangu ajiunge na timu hiyo amefanikiwa kuifungia mabao 4 katika michezo ya ligi kuu.

Habari za uhakika ndani ya Yanga kimetuambia kuwa kabla mshambuliaji huyo hajatua Yanga alitakiwa kujiunga na moja ya klabu kutoka China kwa kiasi cha shilingi bilioni 1.5, lakini dili hilo liliharibika kutokana na uwepo wa janga la Corona.

Hivyo kama wachina hao watamuhitaji tena Sarpong itabidi walipe bilioni 1.2 ili waweze kumpata maana kuna taarifa kuwa bado wachina hao wanamuhitaji Sarpong.

 

 

“Sarpong kabla ya kusajiliwa na Yanga alikuwa akihitajika ndani ya timu nyingi ndani na nje ya Afrika,kuna timu kutoka China ilikuwa tayari kumsajili kwa fedha ndefu zisizopungua Shilingi Bilioni 1.5, lakini dili lao lilikwama kutokana na uwepo wa janga la Corona ila kama kusingekuwepo na janga hilo basi Sarpong angekuwa anakipiga katika moja ya klabu inayoshiriki ligi ya china.

“Wachina bado hawajakata tamaa ya kumuhitaji Sarpong kwani bado wanamfuatilia kwa ajili ya kujaribu kumsajili tena, Yanga wanaweza kumuachia Sarpong lakini itawalazimu kumnunua mshambuliaji huyo kwa shilingi Bilioni 1.2 na kama hawatafikia hapo basi hawatampata,” Kilisema Chanzo hiko.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA KASINO YA MERIDIANBET

Neptune’s Richies ni mchezo Unaokupa pesa chap chap huku ukiwa unaburudika kupitia Kasino ya Mtandaoni ndani ya Meridianbet.

Neptune's-Riches_Casino-Post_30-January

Cheza hapa

11 Komentara

    Vizuri

    Jibu

    Jembe bado sana

    Jibu

    China waweke dau la kutosha wamchukue tu

    Jibu

    Wafanye mpango waweze kumchukua Yuko vizuri

    Jibu

    China kazi ipo

    Jibu

    Sarpong yupo juu

    Jibu

    Hapo yanga wanayumba wanataka kumtoa mchezaji mzuri

    Jibu

    Vizuri

    Jibu

    Big dili kwa Sarpong

    Jibu

    Sawa tu

    Jibu

    Si aende tu

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.