Aston Villa wanaripotiwa kuwa wanajiandaa kumpa Jack Grealish kandarasi yenye thamani ya pauni 200,000 kwa wiki ili kumshawishi Mwingereza huyo aelekeze jitihada zake kwa kilabu.
Mchezaji huyo wa miaka 25 alisaini mkataba mpya wa Pauni 120,000 kwa wiki huko Villa Park msimu uliopita wa kiangazi, na ameendelea kuwa katika hali nzuri msimu huu, akifunga mara saba na kusaidia magoli 12 katika michezo 22 kwenye mashindano yote.
Manchester United ilihusishwa sana na mchezaji huyo wa kimataifa wa England msimu uliopita wa kiangazi na bado wanafikiriwa kuwa na hamu ya kumleta Staa huyo Old Trafford katika hatua fulani baadaye.

Hata hivyo, kwa mujibu wa 90min, wamiliki wa Aston Villa wanajiandaa kuwazuia mabingwa hao wa mara 20 wa Uingereza kwa kumpa Grealish mkataba wa takribani la Pauni 200,000 kwa wiki.
Tottenham Hotspur, Chelsea na Manchester City hapo awali pia wamehusishwa na mchezaji huyo, ambaye ameweka nyavuni mabao sita na asisti 12 kwenye Premier League msimu huu.
Aston Villa iliponea kushuka daraja kutokana na kutofanya poa sana msimu wa 2019-20, lakini kwa sasa ni ya nane katika jedwali la Ligi Kuu, ikiwa ni tofauti ya alama tano tu kutoka kwa Liverpool anayeshika nafasi ya nne akiwa na mchezo mmoja mkononi.
Unaweza kuvuna mkwanja mrefu kadiri uwezavyo kupitia mchezo wa Gold n Rocks kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Ni rahisi! Vigezo na masharti, kuzingatiwa.



Sania
Jack ni mchezaji mzuri
lombo
asante meridianbet kwa habar moto moto
Magdalena
Villa wamefanya Jambo la maana sana
Sarah
Villa wamefanya Jambo jema sana
Lydia Emmanuel Magoti
Villa wa mefanya vizuri sana
Dorophina
Nice update
Ester mmakasa
Hii ni nzuri kwasababu wachezaji wanapata moyo wa kufanya kazi kwa bidii.
Ester mmakasa
Grealish yuko vizuri kiukweli
Sylvester
Grealish ni mchezaji ambae anathamani zaidi ya kuchezea Aston Villa na kwa maoni yangu aende tu kutafuta kandarasi kwingine ili awe mmoja kati ya wachezaji bora kuliko kubaki tu Aston Villa
Rahma
Nice
Angelina
Nice update
Hopemwaikuka
Anafaa kubak
Venerose
Grealish ni mchezaji mnzur