Tuzo ya Mchezaji na Kocha Bora wa Mwezi February EPL.


 

Orodha Ifuatayo ni orodha ya Makocha na Wachezaji wanaochuana kuwania Tuzo ya Mwezi February. Wachezaji 8 wameingia katika kinyang’anyiro hicho;

Joachim Andersen – Mlinzi wa kati na nahodha wa Fulham alikuwa Mchezaji muhimu na Bora Mwezi huo akiisaidia Klabu yake Kuwa na clean sheets nne katika mechi sita na kufungwa mabao matatu tu. Pia alitoa Assist ya goli la Ola Aina Dhidi ya Burnley.

Harvey Barnes – Winga huyo alifunga katika ushindi wa 3-1 kwa Leicester City dhidi ya Liverpool kabla ya Kufunga tena bao na kutoa Assist Kwenye Ushindi wa 2-1 huko Aston Villa. Aliisaidia Klabu yake kushinda mechi tatu kati ya nne za kwanza za mwezi huo.

Joao Cancelo – Amekuwa mchango mkubwa katika ushindi mfululizo kwa Manchester City, akicheza kutoka beki ya kulia kwenda kuwa kiungo. Ushindi dhidi ya Liverpool na Tottenham Hotspur ulikuwa kati ya Mechi zake tano mnamo Februari na clean sheets Mbili.

Bruno Fernandes – Mreno huyo mshindi wa Tuzo hiyo mara 2 alikuwa Katika kiwango cha juu cha kuhusika katika mabao saba mwezi uliopita kwa Manchester United, akifunga na assist mbili dhidi ya Southampton na kufunga dhidi ya Everton, West Bromwich Albion na Newcastle United – Assist Nne na magoli Matatu Jumla Mwezi Februari.

Ilkay Gundogan – Aliendeleza Kiwango Bora Mwezi uliopita kwa Manchester City kwa kufunga mara mbili katika ushindi wa 4-1 huko Anfield, wakati pia akifunga mabao mawili dhidi ya Spurs na assist Pekee Mwezi huo ya Bao la Raheem Sterling Dhidi ya Burnley.

Jesse Lingard – Alifurahia mwanzo mzuri katika kipindi chake cha mkopo huko West Ham United, akifunga mara mbili kwenye mechi yake ya kwanza dhidi ya Villa, akitoa Assist dhidi ya Sheffield United na Man City na kufunga bao dhidi ya Spurs.

Ruben Neves – Kiungo huyo wa Ureno alifunga mabao matatu na assist moja akiwa na Wolves. Alifunga na assist moja katika ushindi wa comeback huko Southampton na alifunga pua dhidi ya Arsenal na Newcastle.

Raphinha – Winga wa Brazil akikipiga Leeds United alifunga bao kali dhidi ya Southampton na pia dhidi ya Everton. Pia alitoa Assist ya bao la Pascal Struijk huko Arsenal na Kuwa Kwenye Kiwango Bora Sana Siku hiyo.

 

Makocha Wanne wametajwa kuwania tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi wa Pili (Februari) ndani ya Premier League.

Nuno Espírito Santo

Nuno aliiongoza Wolves Mwezi Februari bila kufungwa anawania Tuzo hii kwa mara ya pili, comeback ya Kipindi Cha pili katika ushindi huko Southampton na ushindi wa bao moja moja dhidi ya Arsenal na Leeds United – Ana Sare Mbili Katika Mechi Tano Mwezi uliopita.

Pep Guardiola

Manchester City Chini ya Guardiola iliongeza mbio zao za ushindi hadi mechi 14 za ligi na 20 katika mashindano yote kwa mwezi ambao walifunga mabao 10 kwa ushindi maridadi dhidi ya Liverpool, Tottenham na Everton – Mechi Sita, City ilitoa Vipigo game zotee Mwezi huo.

Thomas Tuchel

Tuchel ambaye hajawhi kutwaa Tuzo hii hakufungwa katika mwezi wake wa kwanza kwenye Premier League akiwa na Chelsea, akipata ushindi dhidi ya Spurs, Sheffield United na Newcastle United kabla ya sare mfululizo – Kwenye Mechi Tano Wana Sare Mbili na Ushindi Mara tatu.

Scott Parker

Parker aliiongoza Fulham kupata alama tisa, pamoja na ushindi wa kwanza wa klabu katika Premier League huko Everton. Mfululizo wao huo Bora uliwafanya Kuwa na alama tatu nyuma kufika eneo salama Hadi mwishoni mwa Februari – Katika Mechi Sita, wepoteza Moja tu, Sare tatu na Ushindi Mara Mbili.

Nani Anastahili Tuzo Hii ya Mwezi February?.


Ni Muda wa Kuvuna Mkwanja na Jungle Jim and the Lost Sphinx

Hauihitaji kufikira mara mbili ni mchezo gani utakupatia mkwanja ndani ya kasino za Meridianbet. Jiunge sasa ufurahie Jungle Jim and the Lost Sphinx.

  CHEZA HAPA

10 Komentara

    Safii sana

    Jibu

    Tuchel anasitahili kuwa mshindi wa kocha bora

    Jibu

    Tumche ni kocha mwenye mfano mzuri wa kuigwa

    Jibu

    Tuchele Yuko vizuri

    Jibu

    Tuchel koch

    Jibu

    Jamaa namkubal sana

    Jibu

    Hongera sana

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Hongera sana wote mlioingia kwenye kinyang’anyiro

    Jibu

    Bora apate kocha wa Man u

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.