Desemba 30, 1984 alizaliwa mchezaji wa kimataifa wa kikapu nchini Marekani LeBron James. Kwa sasa nyota huyo anaitumikia klabu ya Los Angeles Lakers katika Ligi Kuu ya Kikapu nchini Marekani (NBA).
Mara kadhaa amekuwa akifananishwa na mkali wa zamani wa kikapu Michael Jordan kutokana na kuchukua mataji mengi katika mchezo huo. Hivi karibuni Shirika la Habari la Associated Press (AP) limemtaja LeBron James kuwa ni mchezaji bora kwa miaka 10.

Nyota huyo ametwaa mataji matatu ya NBA, mara nne akichukua tuzo ya MVP, mara tatu akichukua tuzo ya MVP katika fainali za NBA na medali mbili za dhahabu katika olimpiki.
LeBron James amecheza katika fainali 15 za NBA All-Star Games na pia akichukua tuzo mara tatu ya MVP katika NBA All-Star.

Alishinda tuzo ya ufungaji bora wa zama zote pia anaongoza kwa ufungaji katika mechi za mtoano katika NBA, James pia ni wa nne kwa kuwa na pointi nyingi katika historia ya NBA. Pia James anashika nafasi ya tisa kwa kutoa pasi za mwisho kwenye historia ya NBA.
Nyota huyo ameitwa mara 12 katika kikosi cha kwanza cha All-NBA First Team na mara tano katika kikosi cha Defensive kutokana na uimara wake wa kuzuia mashambulizi. Nyota huyo alizaliwa Akron, Ohio kwa Gloria Marie James na baba yake Anthony McClelland. Wakati anazaliwa mama yake alikuwa na umri wa miaka 16.
James amekulia katika familia ya kimaskini nchini humo, baba yake alikuwa mtu wa matukio kila wakati alikuwa mikononi mwa polisi hali iliyoyumbisha sana familia yao.
Mama yake hakuwa na kazi maalumu hivyo alipambana kwa kila hali kuhakikisha James anastawisha licha ya hali ngumu ya kimaisha. Alianza kucheza kikapu katika daraja la tano.
Maana Kamili ya Ushindi Katika Kasino za Meridianbeti ni Pamoja na Mchezo wa Tropical Wild.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Tropical Wild na uwe moja ya washindi na Mabingwa.



Hopemwaikuka
Historia nzur
Lydia Emmanuel Magoti
Historia iko poa hii
Caroline
Lebron ni mchezaji mzuri sana
Sarah
Historia iko vizuri
Venerose
Lebron bado kijana mdogo
Adelta
History yake ni nzuri na yeye bado ni kijana mdogo lazima ndoto zake zitimiye
Dorophina
James ni mchezaji mzuri sana
warda
Namkubali sana James