Droo ya Robo fainali ya Ligi ya Mabingwa imetoka siku ya leo Ijumaa Ambapo timu ya Chelsea imepangwa kukutana na FC Porto wakati ya Manchester City watawaongoza Borussia Dortmund.

Liverpool wamepangwa kumenyana na Real Madrid katika robo fainali wakati pia tutashuhudia timu mbili zilizokutana katika fainali ya Champions League msimu uliyopita Bayern Munich na Paris Saint-Germain zikikutana tena.
Manchester City ya Pep Guardiola itakuwa katika mawindo yake ya kuleta taji ya Champions League kwa mara ya kwanza katika huko Etihad Stadium watakuwa na kibarua cha kuwasimamisha Jadon Sancho na Erling Haaland ambao wamekuwa na muunganiko mzuri katika timu ya Borussia Dortmund.
Paris Sain-Germain watakuwa katika mawazo ya kulipiza kisasi kwa Bayern Munich baada ya kupokea kipigo cha 1-0 katika fainali ya UCL 2020 goli pekee lililofungwa na Kingsley Coman.
Michezo ya kwanza ya robo fainali imepangwa kuchezwa April 6 na 7 na mechi za marudiano zitachezwa wiki moja baadaye.
Droo kamili ya robo fainali ya Ligi ya Mabngwa:
Manchester City vs Borussia Dortmund
Porto vs Chelsea
Bayern Munich vs PSG
Real Madrid vs Liverpool
Maana Kamili ya Ushindi Katika Kasino za Meridianbeti ni Pamoja na Mchezo wa Tropical Wild.
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Tropical Wild na uwe moja ya washindi na Mabingwa.



Adelta
Tunasubiri dakika90
Hopemwaikuka
Bonge moja la mech
Lydia Emmanuel Magoti
Moja tuone
Caroline
Kila la kheri
Sarah
Bonge la mechi
Venerose
Mmmh nasubir tuone Mambo yatakuaje
Dorophina
Mechi itakuwa kali htr dakika 90 ndio muamuzi
warda
Nawaombea hawa Chelsea wapigwe tu