Neymar: Suala la Mkataba Mpya Siyo Ishu!

Nyota wa PSG, Neymar amesema suala la mkataba wake mpya na PSG sio ishu na anahisi kuendelea kuwa na furaha klabuni hapo kuliko wakati mwimgine wowote. Neymar amezungumza hayo baada ya PSG kufuzu hatua kwenda nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Nyota huyu, ambaye aliwasili PSG akitokea Barcelona kwa €222m mwaka 2017, mkataba wake wa sasa unafika mwisho mwakanni 2022. Pande zote zilitajwa kuwa kwenye majadiliano ya mkataba mpya, mpaka pale Neymar aliporipotiwa kusitisha mazungumzo ya mkataba mpya.

Staa huyu alikuwa anahusishwa na kurejea La Liga, lakini PSG wao wamesisitiza kuwa Neymar hatakuwa sokoni, hata kwa pesa nyingi hawako tayari kumuuza kwa sasa.

Hata hivyo, alipoulizwa juu ya hali yake ya mkataba mpya amebainisha hilo sio tatizo kwa sasa. Akizungumza na ESPN Brazil amenukuliwa akisema;

“Kusaini mkataba mpya, sio tatizo kwa sasa. Kimsingi nahisi kuwa huru na kuwa nyumbani hapa PSG. Nahisi kuwa na furaha kuliko wakati wowote”


 

JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

CHEZA HAPA

 

4 Komentara

    Neymar kwa sasa anaifurahiya timu yake kutokana na matokeo mazuri wanayoyapata , hivyo swala ya yeye kutaka kuhama hajalipa kipao mbele.

    Jibu

    Neymar uko makini

    Jibu

    Neymar yuko vizuri

    Jibu

    Huyu dogo yupo mguu mmoja mnje mmoja ndani

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.