Onyango: Tutaleta Champions League Nyumbani

Beki wa Simba Joash Onyango amesema ndoto yao kubwa ni kuhakikisha wanaleta nyumbani taji la Caf Champions League.

Miamba hao wa msimbazi wamefurahia muendelezo mzuri kwenye kampeni hii wakiwa tayari wamekata tiketi ya robo fainali kutoka kwenye kundi gumu sana Kundi A ambalo lilikuwa na timu kama Al Ahly ya Misri, AS Vita ya DRC na Al Merrikh ya Sudan.

Simba wamejongea kwenye robo fainali wakiwa ndiyo viongozi wa kundi lao kwa jumla ya alama 13 wakati Al Ahly wakiwa nafasi ya pili kufuzu hatua ya nane bora.

Simba wakiwa wanasubiri droo ambayo imepangwa kufanyika April 30 mlinzi wa Kenya ambaye alijiunga na Simba akitokea Gor Mahia ya FKF Premier League ameeleza lengo lao la kushinda taji la Champions League.

“Ni ndoto ya kila mchezaji kuapata mafanikio na hiyo ndiyo sababu wachezaji wa Simba wamekuwa wakipambana tangu tulipoweka lengo la kushinda taji la Caf na kulileta nyumbani, tunaamini itakuwa hivyo,” Onyango alisema akinukuliwa na Nation Sport.


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

CHEZA HAPA

4 Komentara

    Tunawatakia kika la kheri

    Jibu

    Tunazidi kuwaombea ili ndoto yenu itimiye

    Jibu

    Kila lakheri kwao

    Jibu

    Nakubali sana maneno yake

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.