Ligi ya Mataifa UEFA inaanza kutimua vumbi leo hii na gemu ya kwanza ni kati ya Ufaransa na Ujerumani ambao ni Mabingwa wa Makombe ya Dunia yaliyopita. Kwenye gemu 29 zilizopita taifa la Ufaransa limeshinda mara 13, Ujerumani wakishinda mitanange 9 na kutoka suluhu gemu 7. Taifa la Ufaransa limefanikiwa kuitandika Ujerumani jumla ya magoli 47 na Ujerumani nao wamewachapa goli 45!
Maneno ya makocha
Joachim Löw amesema kwamba yeye atawapa nafasi wachezaji wachanga na wale wenye uwezo mkubwa. Na pia amethibitisha kwamba hana kabisa mpango wa kuzungumza na Ozil juu ya uwezekano wa yeye kurejea kwenye timu yake ya taifa na pia kocha huyo ambaye aliwaongeza wasakata kabumbu kadhaa kikosini wakiwemo mchezaji wa PSG, Thilo Kehrer, Nico Schulz wa Hoffenheim na kinda wa Bayer Leverkusen, Kai Havertz huku naye Leroy Sane akirudi kikosini tena!
Naye Bwana Didier Deschamps ameweka wazi kwamba kwa wao kunyanyua ubingwa wa dunia sio mzigo kwake na kuwa wao wamejipanga mahususi kushindana na kupambana haswa wawapo dimbani. Amesema kuwa yeye anapenda sana mechi za ushindani na hawezi kabisa kuibeza Ujerumani kwa sababu walitoka hatua ya makundi na kwamba bado anaamini kuwa ile ni timu bora sana.
Vikosi
Ujerumani: Neuer (c) – Kimmich, Boateng, Hummels, Schulz – Gündogan, Kroos – Müller, Reus, Sane – Werner
Benchi: ter Stegen, Ginter, Kehrer, Rüdiger, Schultz, Süle, Tah, Brandt, Draxler, Goretzka, Havertz, Petersen
Kocha: Joachim Löw
Ufaransa: Lloris (c) – Pavard, Varane, Umititi, Hernandez – Pogba, Kante – Mbappe, Griezmann, Matuidi – Giroud
Benchi: Costil, Areola, Rami, Sidibe, Mendy, Kimpembe, Tolisso, Nzonzi, Fekir, Dembele, Lemar, Thauvin
Kocha: Didier Deschamps



Mariam mtandama
Duuuh
Issa
Ufaransa wababe kwa mpira na kwa rekodi
Lydia Emmanuel Magoti
Ufaransa wababe kwampira kuleta lekodi nzuri
Povel
France noma sana hiiiii