Chelsea Wamtamani Elliot, Mtoto wa Miaka 15

Klabu ya chelsea wameripotiwa kuvutiwa na mtoto machachari Harvey Elliott mwenye umri wa miaka 15 kutoka katika shule ya mpira wa miguu ya vijana pale Fulham. Chelsea wameonyesha kuvutiwa na mchezaji huyo mtoto ambaye klabu nyingi zinamtamani.

Evining Standars wameripoti kuwa Bosi wa Chelsea Slavisa Jokanovic ametamani kumsajili mchezaji huyo, lakini kwa mujibu wa sheria za Shirikisho la Mpira wa Miguu FA kinda huyu hawezi kufanyiwa mazungumzo ya biashara mpaka atakapofikisha umri wa miaka 17.

Kinda huyo amefanya vyema katika michezo yake ya shule ya vijana na kupata mualiko wa kujifunza katika kikosi kikubwa cha Slavisa Jokanovic. Maendeleo ya kinda huyo hayawezi kufichika kulingana na uwezo wake.

Barcelona walionyesha pia kuvutiwa naye mapema wakiungana na Manchezter City. Mpaka sasa ni Barcelona, chelsea , Man City na Borussia Dortmund ambao wanammezea mate kinda huyo wa Fulham.

4 Komentara

    Wamchukue tu kijana huyo atawasaidia badae.

    Jibu

    Chelsea mchukuen kinda hilo

    Jibu

    Chelsea mchukuen huyo atawasadia badae

    Jibu

    wanachukua sana watoto ndio mana wanafungwa sna

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.