Klabu ya chelsea wameripotiwa kuvutiwa na mtoto machachari Harvey Elliott mwenye umri wa miaka 15 kutoka katika shule ya mpira wa miguu ya vijana pale Fulham. Chelsea wameonyesha kuvutiwa na mchezaji huyo mtoto ambaye klabu nyingi zinamtamani.
Evining Standars wameripoti kuwa Bosi wa Chelsea Slavisa Jokanovic ametamani kumsajili mchezaji huyo, lakini kwa mujibu wa sheria za Shirikisho la Mpira wa Miguu FA kinda huyu hawezi kufanyiwa mazungumzo ya biashara mpaka atakapofikisha umri wa miaka 17.
Kinda huyo amefanya vyema katika michezo yake ya shule ya vijana na kupata mualiko wa kujifunza katika kikosi kikubwa cha Slavisa Jokanovic. Maendeleo ya kinda huyo hayawezi kufichika kulingana na uwezo wake.
Barcelona walionyesha pia kuvutiwa naye mapema wakiungana na Manchezter City. Mpaka sasa ni Barcelona, chelsea , Man City na Borussia Dortmund ambao wanammezea mate kinda huyo wa Fulham.


Furahav
Wamchukue tu kijana huyo atawasaidia badae.
Issa
Chelsea mchukuen kinda hilo
Lydia Emmanuel Magoti
Chelsea mchukuen huyo atawasadia badae
amon
wanachukua sana watoto ndio mana wanafungwa sna