Sarri Amekutana na Kazi Ngumu Chelsea

Bosi wa Chelsea Mourizio Sarri, anaamini kuwa amekutana na kazi ngumu sana Chelsea. Bosi huyu mwenye umri wa miaka 59, ambaye amewahi pia kuwa bosi wa  Napoli, anadai kuwa kazi ya Chelsea haiwezi kufananishwa na kazi aliyokuwa anaifanya Napoli, Kazi ya hapo ni ngumu zaidi.

Sarri alifika Stanford Bridge July mwaka huu, akichukua nafasi ya Antonio Conte. Alitokea Napoli ambao walimteua Ancelotti kuwa mrithi wake, akiwa Napoli hakufanikiwa kupata Kombe katika misimu yake mitatu aliyokuwepo huku Conte aliyemuachia kijiti Chelsea akiwa ameweza kupata taji la Premier League na FA kwa kipindi alichoitumikia Chelsea.

Bosi huyu anakiri kuwa kazi aliyoikuta chelsea ya kuendeleza alipoacha Conte sio rahisi, anatakiwa kufanya jitihada za ziada, anasema “sikushinda chochote Napoli, lakini Conte alishinda hapa sio rahisi kuchukua nafasi yake”.

Chelsea chini ya uongozi wake wamefanikiwa kuanza vyema Premier League wakiwa hawapigiki kwa kushinda gemu zote wakati Napoli wamepoteza gemu 1 wamepigwa kipigo cha 3-0 kutoka kwa Sampodoria kwenye Serie A.

4 Komentara

    Pambana sasa.

    Jibu

    Jitahidi uweke sawa

    Jibu

    Pambana sana

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.