De Zerbi Amesanda kwa Juventus

Kocha wa Sassuolo Roberto De Zerbi  amekiri kuwa Juventus ndio wababe wa Italia na Ulaya huku akisisitiza kuwa hiyo haimaanishi kuwa tayari wamewashindwa.

Sassuolo wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya Serie A baada ya kucheza gemu 3 na kushinda mbili huku wakitoa sare gemu moja. Juventus ndio wanaongoza msimamo wa ligi kwa pointi 9, pointi mbili mbele ya Sassuolo baada ya kushinda gemu zote tatu.

Kocha wa Sassuolo anasema anafikiria namna wanavyoweza kumshinda Juventus, akikiambia chanzo cha habari cha Italia cha Corriere dello Sport, alisema “Juventus wana nguvu zaidi kwa upande wa Italia, pia wana nguvu zaidi Ulaya katika msimu huu”

Roberto anadai anaangalia namna ya kuwazuia wababe hao, anaamini wataweza japokuwa hajui ni namna gani. Hata hivyo, anajivunia kuwa nafasi ya pili nyuma ya Juve. Kwakuwa anaamini bado hawajashindwa, basi ataonyesha jitihada zote kuhakikisha wanawakalisha wababe hao.

5 Komentara

    Mmh juve pakubwa sana

    Jibu

    duuh juve wanamkwara sawa acha tuone

    Jibu

    Juve noma sana

    Jibu

    Juventus kiboko

    Jibu

    Iko juu juve.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.