EURO 2020 na Matokeo ya Kushangaza.

Mambo yanazidi kunoga katika michezo ya hatua ya 16 bora kwenye Euro 2020. Hakika matokeo ya baadhi ya michezo, yanashangaza!

Nani aliwaona Czech Republic wakiwatoa Uholanzi au Croatia vs Spain kuchezwa dakika 120? Hakika soka ni mchezo wa nafasi, lolote linaweza kutokea viwanjani.

Ikiwa imesalia michezo 2 tu ya hatua ya 16 bora kwenye Euro 2020, michezo 6 ya mwanzo imetoa taswira mpya katika mashindano haya.

Mpaka sasa, robo fainali ni Italia vs Ubelgiji, Denmark vs Czech Republic, Hispania vs Switzerland. Hakina Ureno, Uholanzi wala Ufaransa kuelea hatua ya robo fainali. Nani kuungana nao?

Mashabiki wa soka walipigwa na butwaa kwa muda baada ya kuona Ufaransa (Bingwa wa Dunia) akitolewa jasho na Switzerland kwenye mchezo wao jana usiku. Licha ya kuongoza kwa magoli 2, dakika 10 ziliwatosha Switzerland kupindua meza na dakika 90 kumalizika kwa matokeo ya 3-3.

Dakika 30 za muda wa ziada hazikutosha kuamua mshindi na mikwaju ya penati ikahusika. Sommer alikuwa shujaa wa Switzerland baada ya kuokoa penati ya Kylian Mbappe na kupeleka machungu kwa mashabiki na timu ya Taifa ya Ufaransa kwa ujumla.

Leo ni zamu ya Ukraine vs Sweden huku Uingereza akichuana na Ujerumani, washindi wa michezo hii watachuana kwenye robo fainali. Tutegemee matokeo mengine ya kushangaza kwenye mchezo huu. Hakika Euro 2020, haina mwenyewe!


KUSANYA PESA HAPA!

IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!

United, United Wakutana na Mawakala wa Camavinga, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.