Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Congo DRC, Florente Ibenge ameamua kuachana na klabu ya AS Vita inayoshiriki ligi ya nchi hiyo baada ya kuhudumu klabuni hapo kwa takribani miaka 9.
Kitendo cha AS Vita kuachana na Ibenge kinalandana kabisa na kile cha Ujerumani kuachana na Joachim Low ambaye ameachana na timu ya taifa ya Ujerumani baada ya kuhudumu taifa hilo kwa takribani miaka 15.
Taarifa rasmi kutoka kwenye Uongozi wa timu hiyo zinaeleza kuwa Ibenge ameachana na klabu hiyo rasmi leo hii.
“ ndugu mashabiki, ninatangaza kuondoka kwa kocha wetu Jean-Florent. Kwa niaba ya klabu ya AS Vita, tunamshukuru kwa utumishi wake na tunamtakia kila la kheri.” – Bestine, Rais AS Vita
Florente anaondoka AS Vita akiwa kama kocha mwenye mafanikio mengi sana katika timu ya AS Vita, lakini mwaka huu hakufanikiwa baada ya alama zake tisa kuondolewa baada ya kunyang’anywa kutokana na kumchezesha mchezaji asiye halali.
IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!

