Sergio Ramos anaripotiwa kuwa tayari ameshawasili Paris, akijiandaa na kusaini mkataba na miamba wa Ligue 1 Paris Saint-Germain.
Ramos kwa sasa ni mchezaji huru tangia alipomaliza mkataba wake mwanzoni mwa mwezi huu na Real Madrid, na ikawekwa wazi kuwa PSG ndiyo klabu iliyokuwa na nafasi kubwa ya kumsaini nyota huyu.
Nyota huyu wa zamani wa Real Madrid ametajwa kuwepo kwenye mazungumzo na klabu ya PSG kwa takribani wiki kadhaa na sasa wanaonekana kuwa kwenye sehemu nzuri ya mazungumzo hayo.

Kwa mujibu wa Mundo Deportivo, Ramos amesafiri kuelekea Paris kwa ajili ya kukamilisha dili lake alilokuwa kwenye mazungumzo na PSG.
Inaripotiwa kuwa ofa ya ramosi inahusisha mkataba wa miaka miwili, baada ya kushindwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja na Real Madrid.
Nyota huyu mwenye umri wa miaka 36 alibainisha kuwa alikuwa tayari kusaini mkataba wa mwaka mmoja na Real Madrid, lakini bahati mbaya alifikia maamuzi ya kukubali wakati Real Madrid wao wakiamua kuiondoa ofa hiyo mezani.
IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!


Issa
Bek bora