Nyota wa Barcelona na Argentina Lionel Messi amewatumia ujumbe wa onyo wachezaji wenzake wa timu ta Taifa juu ya Neymar kuelekea fainali ya Copa America.
Messi na wanatimu wenzake walipenya kuingia kwenye fainali ya Copa America baada ya kushinda kwa penati dhidi ya Colombia.
Argentina walianza kwa kuwachapa bao la mapema Colombia kupitia Lauturo Martinez kabla ya Luis Diaz kusawazisha na kulazimisha wacheze hadi mda wa nyongeza na hatimae mashuti ya penati.
Kufika fainali kwa Argentina ni nafasi ya Leo kushinda taji kubwa akiwa na timu yake ya taifa lakini kibarua kilichopo ni kuruka kiunzi cha Brazil ambao wapo pamoja na mwanatimu mwenzake wa zamani Neymar Jr.
Kuelekea fainali Jumapili hii, Messi amewaambia Argentina kuwa Brazil wakiwa na Neymar watakuwa wagumu sana na wanahitaji kujiandaa kwa sababu ya hilo.
“Brazili wakiwa na Neymar watakuwa wagumu sana, tunamfahamu uwezo wake na kile anachoweza kukifanya binafsi”
Lionel Messi
IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!
Issa
Kitaelewka tu