Timu ya Simba SC ya Tanzania imewekewa gwaride la heshima kwa kutoa ubingwa wa VPL mwaka 2020/2021, Kama ilivyo ada kwenye soka, bingwa wa ligi husika atapewa gwaride la heshima endapo atatangazwa bingwa kabla ya ligi kutamatika.
Mechi ya raundi ya 33 kati ya Simba na Azam ilikuwa ni ya damu na jasho na kisasi ambapo Simba walionekana kutomiliki mpira sana kutokana na kukatika kwa eneo la kiungo.
Azam walitawala mpira kwa kipindi cha kwanza chote lakini kuingia kwa Erasto Nyoni, Rally Bwalya na Chris Mugalu kulileta afadhali kwa vijana wa Gomes ambao walianza kushambulia kwa kueleweka mpaka pale Kagere alipofunga goli la kusawazisha.

Matokeo hayo yanaifanya wanamsimbazi kufikisha alama 80 huku Azam wakiwa na alama 65, kati ya wachezaji wote Idd Nado ndo amekuwa akifanikiwa kufunga magoli manne katika mechi tatu za mwisho.

Vijana wa Gomes watacheza mechi ya mwisho dhidi ya Namungo tarehe 18 na siku hiyo hiyo watakabidhiwa Kombe lao.
Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!


