Real Madrid Kumtazama Salah Kama Mbadala wa Mbappe

Meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti anaripotiwa anataka klabu hiyo ihamie kwa mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah ikiwa mpango wa Kylian Mbappe hauwezi kukamilika.

Mbappe bado hajakubali mkataba mpya huko Paris Saint-Germain na anastahili kuwa mchezaji huru katika kipindi cha miezi 12 ijayo, lakini kuna hofu kwamba Real Madrid bado wanaweza kukwamishwa na bei.

Hata hivyo, raisi wa Los Blancos Florentino Perez ameripotiwa kuwa na nia ya kumleta mshambuliaji mpya pale mji mkuu wa Uhispania msimu huu wa joto, ina maanisha kuwa njia mbadala ya Mbappe lazima itafutwe.

Salah hapo awali alikanusha kuhamia Real Madrid au Barcelona, ​​na Fichajes anadai kwamba Ancelotti anataka kumleta mshambuliaji huyo wa Misri klabuni hapo msimu huu wa joto.

Mchezaji huyo wa miaka 29 anafikiriwa kuwa yuko kwenye mazungumzo juu ya kuongeza mkataba wake pale Anfield ambao unamalizika mwaka 2023, lakini Liverpool wanasemekana kuwa wanazingatia uwezekano wa kumpata winga wa kulia wa Italia Domenico Berardi.


JIUNGE NA FAMILIA YA MABINGWA!

Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!

Italia, Italia Bingwa Euro 2020., Meridianbet

JIUNGE SASA!

2 Komentara

    Klopp atakubali kweli kumuachia Salah

    Jibu

    Madrid mbinu zao wambebe huru

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.