Manchester City Hawana Bahati kwa Lewandowski

Manchester City wanaripotiwa kuwa ‘hawana nafasi’ ya kumpata Robert Lewandowski wa Bayern Munich msimu huu wa joto.

Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 dimbani Allianz Arena unastahili kumalizika mwishoni mwa msimu wa 2022-23, na awali alikuwa amekataa kukanusha uhamisho kwenda ligi nyingine.

Man City wanatarajiwa kuweka Harry Kane kama kipaumbele kwa msimu huu wa joto, lakini ikiwa watapewa bei kubwa ya uhamisho wa nahodha huyo wa England, kuelekeza nguvu kwa Lewandowski.

Manchester City Hawana Bahati kwa Lewandowski

Hata hivyo, chanzo kutoka Ujerumani kinadai kuwa hakuna ‘nafasi’ ya Lewandowski kuondoka Bayern katika wiki zijazo, licha ya hali yake ya mkataba kutokuwa na uhakika.

Bayern inadaiwa wanaamini kwamba wakala wa Lewandowski, Pini Zahavi anafanya ujanja ujanja katika jitihada za kuongeza mshahara wa mshambuliaji huyo, na meneja Julian Nagelsmann amekiri kuchanganywa na dhana ya kinachoendelea juu ya nyota wake.

Lewandowski alifunga mabao 41 katika michezo 29 ya Bundesliga muhula uliopita, akivunja rekodi ya awali ya wakati wote ya magoli 40 iliyowekwa na Gerd Muller msimu wa 1971-72.

2 Komentara

    Bayern hawawezi kumuachia kirahsi hasa katika kipindi hiki

    Jibu

    Man city wajipange

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.