Hakika Man United wamejaribu kuonesha umwamba wao kwenye soko la usajili, hili ni suala ambalo lilishaanza kusahaulika kwa miaka ya karibuni.
Kwa siku za hivi karibuni, United wamekuwa wakisemwa vibaya kwa kushindwa kuonesha ubora wao wa kiuchumi kwenye madirisha kadhaa ya usajili yaliyopita. Ed Woodward, amekuwa akinyooshewa vidole kwa kushindwa kusajili wachezaji kwa mikakati na pengine kwa muda sahihi.
United imekuwa ikisajili wachezaji kuelekea mwishoni mwa dirisha la usajili, suala ambalo halikuwa limezoeleka wakati wa Sir Alex Ferguson. Mwaka huu mambo yamekuwa tofauti, Man United imeshawasajili wachezaji watatu wakati dirisha la usajili likiwa limebakiza mwezi mmoja kuhitimishwa.
Tom Heaton, Jadon Sancho na Rafael Varane (bado kukamilisha vipimo) ni wachezaji watatu wanaojiunga na United kuelekea msimu ujao. Hakika Ole anakila sababu ya kujivunia kwa hili.

Japokuwa, ripoti mbalimbali zinasema United hawatoishia hapa pekee. Kuna uwezekano wa kusajili beki wa pembeni pamoja na kuboresha safu ya kiungo kwenye majira haya haya ya usajili.
Hili litawezekana endapo hatma ya Paul Pogba itajulikana klabuni hapo wakati huu huu wa usajili. Pogba amegoma kusaini mkataba mpya na Man United na akiwa amebakiza mwaka 1 pekee -mkataba wake kumalizika, Pogba anahusishwa na PSG ambayo bado haijatoa dalili yeyote ya kutaka kumsajili mchezaji huyo majira haya.
Endapo Pogba atauzwa kwa klabu yeyote inayomtaka kwenye majira haya, United watakuwa na nafasi ya kusajili mchezaji/wachezaji wengine kutokana na mapato watakayopata kwenye usajili huu. Kama Pogba atabaki, basi huenda United wasisajili mchezaji mwingine yeyote kwenye dirisha hili la usajili labda kama Ole Gunnar Solskjaer atauza wachezaji kadhaa ili apate pesa za usajili.
SHOOT! mchezo unaokupa nafasi ya kupambania ushindi wako mkubwa kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet! Usisubiri hii, jiunge sasa kufurahia ushindi!



Ernest
Sio Mbaya ni wakati sasa wa kuachana na Pogba
Angelina
Itakuwa vizuri