Mbilinge mbilinge za dirisha la usajili, zilitawaliwa na sakata la Harry Kane kuondoka Spurs. Declan Rice, amejifunza kitu katika hili. Hafikirii kufanya makosa kama ya Kane.
Rice alijikuta akilazimika kusalia West Ham United licha ya baadhi ya timu (Chelsea na Man United) kutaka kumsajili bila ya mafanikio. Japokuwa aliamini, ulikua ni muda sahihi kwake kuondoka, The Hammers waliweka dau la £100M ili wamuachie. Hakika Declan aliona dhahiri hii ni nafasi aliyobaniwa na West Ham.
Harry Kane alijikuta akigonga mwamba kwenye juhudi zake za kutaka kuondoka Spurs akiamini alikua na makubaliano (ya mdomo) na Daniel Levy kuwa angeruhusiwa kuondoka kwenye dirisha kubwa la usajili.

Man City walitoa kitita cha takribani £125M ili kumsajili Kane lakini haikuwezekana. Hakika, mkataba wa maandishi ndio kitu pekee kinachoweza kutumika kama marejeo ya makubaliano na sio maneno ya mdomo tu.
Rice amebakiza miaka 3 kwenye mkataba wake na West Ham United na imeripotiwa kuwa, mchezaji huyo hatosaini mkataba mpya kama mkataba huo (mpya) hautawekwa kipengele cha kumruhusu kuondoka klabuni hapo kwa dau atakaloliridhia. Hakika nahodha huyu wa The Hammers amejifunza, Kane alikuwa na makubaliano ya mdomo tu na haikuwezekana kuondoka bila kuonesha makubaliano ya maandishi.
Hakika, mwenzako akinyolewa – zako tia maji.
BADILI KILA KITU KWA SARAFU MOJA TU!
Unaweza kutengeneza faida kubwa huku ukiwa unaifurahia safari kabambe ya wacheza sarakasi kupitia sloti mpya ya Circus Fever Delux kupitia Kasino ya Meridianbet pekee Dau lako linaweza kukupa pesa maradufu kupitia kete au sarafu.



[email protected]
Nice update