Klabu ya Simba SC imelazimika kuzindua jezi mpya kwaajili ya msimu 2021-22 baada ya kusemekana kwamba jezi hiyo imevuja hivyo kwa maswala ya kibiashara ni lazima irasmishe kwaajili ya kuingia sokoni.
“Maombi ya jezi kutoka kwa Mashabiki wa Simba yamekuwa makubwa sana na uongozi umeona ni vyema kuwasikiliza, natangaza rasmi kwamba kuanzia sasa jezi mpya za Simba zinapatikana sasa kwenye maduka ya Vunja Bei Nchi nzima.
“Mashabiki wana hamu wameona Jumamosi mbali, kwahiyo kesho ratiba za uzinduzi zitaendelea kama kawaida lakini jezi tayari zimeanza kuuzwa” alisema Ezekiel Kamwaga katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea siku ya Wekundu wa Msimbazi itakayofanyika siku ya Jumamosi.
“Hili suala la jezi kuvuja sio jambo la ajabu, jezi za Chelsea na Man City zilivuja, nimeona kuna Watu wanashabikia jezi kuvuja, tuna Mwekezaji ame- invest Bil 2 kwenye jezi, inashangaza kuna Watu mashuhuri wengine Viongozi wanashabikia jezi kuvuja kitendo ambacho sio cha kiungwana”
“Utani wa jadi wa kuvujishiana jezi tunapokwenda utakuwa sio utani wa jadi itakuwa vita”
“Mzigo umefika, jezi bora, jezi ya viwango, jezi ambayo inafaa kuvaliwa na kila Mwanasimba na mpenda soka popote pale duniani”
BADILI KILA KITU KWA SARAFU MOJA TU!
Unaweza kutengeneza faida kubwa huku ukiwa unaifurahia safari kabambe ya wacheza sarakasi kupitia sloti mpya ya Circus Fever Delux kupitia Kasino ya Meridianbet pekee Dau lako linaweza kukupa pesa maradufu kupitia kete au sarafu.



[email protected]
Safi sana