Man United wnaripotiwa kuwa wanapanga kuachana na wachezaji kama saba katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari.
Mashetani Wekundu waliteka dirisha la usajili la hivi karibuni la uhamisho na kwa kumrejesha tena Cristiano Ronaldo, wakati Jadon Sancho na Raphael Varane pia wakiwa sehemu ya usajili Mashetani Wekundu.
Hata hivyo, wachezaji wakubwa walioondoka walikuwa machache sana kwa upande wa Ole Gunnar Solskjaer, wakiachana na Sergio Romero na Daniel James aliyekwenda Leeds United.

Huku United ikidhaniwa kuwa kuwa inapanga uhamisho wa pesa nyingi kwa Declan Rice au Jude Bellingham katika msimu wa joto wa 2022, The Sun inaripoti kwamba wachezaji saba wasio na nafasi kubwa kwa sasa wanaweza kuondoka kwenye dirisha lijalo la uhamisho.
Ripoti hiyo inawataja Donny van de Beek, Jesse Lingard, Diogo Dalot, Phil Jones, Eric Bailly, Anthony Martial na Alex Telles kuwa wanaweza kuondoka, na United wamekaa na kila mchezaji kujadili hatma yao kabla ya mwisho wa mwaka.
Lingard alitarajiwa kukamilisha uhamisho wa kudumu kwenda West Ham United msimu huu wa joto, ingawa hivi karibuni Solskjaer alidai kwamba Mashetani Wekundu wanafanya mazungumzo na mshambuliaji huyo juu ya mkataba mpya.
Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii.!


