Maridhiano: Fury na Wilder

Hali inazidi kuwa nzuri upande wa mashabiki wa masumbwi duniani juu ya ripoti zinazoendelea kuhusu pambano kubwa na lenye hadhi ya juu kati ya wapiganaji bora duniani ambao ni Tyson Fury [30] raia wa Uingereza ambaye amekuwa akiburuza wapinzani wake mara kwa mara ulingoni, kitu kinachomfanya aendelee kujiwekea rekodi nzuri ya kutwaa mikanda yenye hadhi ya juu ; ambapo ataumana na bondia Deontay Wilder [33].

Wawili hawa walikutana kabla ya mwaka mpya -Desemba, huku ikishuhudiwa Mmarekani Wilder akiondoka na mkanda wake baada ya maamuzi ya mshindi kutopatikana katika pambano hilo dhidi yake na Muingereza huyo [50-50]; katika pambano lililokuwa la kuvutia na la aina yake katika historia ya masumbwi.

Promota wa Fury, Frank Warren yupo katika hatua ya kuwezesha pambano hili liweze kutokea kwa kujaribu kuweka mazungumzo ya karibu na uongozi wa Wilder ili kuweza kuweka mambo sawa kuona njia sahihi ya mabondia wao kuweza kurudi ulingoni kwa mara nyingine ili kupata mshindi: mara baada ya mshindi kutopatikana kwenye pambano lililopita kati ya wawili hao wenye heshima kubwa duniani.

Warren anadhihirisha kwamba pambano hilo lazima litokee kwa sababu hadi sasa anafanya mawasiliano na Shelly Finkel ambaye ni meneja wa Wilder kusudi waweze kuafikiana juu ya wapi na lini pambano hili liweze kupiganiwa. Ikumbukwe wawili hawa wana historia ndefu sana katika masumbwi na ni wapiganaji wenye hadhi ya uzito wa juu wenye mataji makubwa na mikanda yenye hadhi ya dunia.

Pamoja na kwamba pambano hilo haliwezi kuzuilika kutokana na matokeo yaliyopatikana hapo awali, kuna taarifa za chini zinazoendelea kwamba mwanamasumbwi mwenye damu ya Kiafrika, Antony Joshua [29] anaonekana kutaka pambano na Wilder ili waweze kupimana ulingoni na kujiwekea heshima zaidi. Joshua anashikilia rekodi kubwa duniani ikiwa ni zile za WBA, IBF na WBO ambazo amejizolea ndani ya kipindi kifupi sana tangu awe mwanamasumbwi.

Pamoja na taarifa hizo inaonekana Fury bado anania ya kutaka kukutana kwa mara nyingine na Wilder ili aweze kuchukua mkanda unaomilikiwa na mpinzani wake. Imani hii inaelekea kutokea kama inavyokusudiwa kwa sababu hadi sasa pambano lao linaonekana ndilo lenye uzito zaidi ya hilo la Joshua linalozungumziwa hadi sasa, kwamba huenda likavuruga ratiba ya pambano linaloshughulikiwa na Frank Warren.

Kwenye historia yake Fury, katika mapambano 28 aliyopigana ya kiwango chake ameshinda 27 na kusuluhu moja ambalo ni dhidi ya Wilder; huku mpinzani wake aliyepigana naye anashikilia rekodi ya WBC tangu mwaka 2015, pia akiwa ni Mmarekani wa kwanza kufikia rekodi ya kuwa mshindi wa mkanda wa dunia katika miaka tisa ambayo taifa hilo lilikaa bila kuwa na mkanda huo.

4 Komentara

    Hongera sana kwa mchezo wa masumbwi

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Don’t miss

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.