Meneja wa zamani wa Inter Milan, Antonio Conte amesema klabu ya Chelsea wameshindwa kutambua jinsi gani wanaweza kumtumia mshambuliaji wao Romelu Lukaku.

Lukaku alikuwa akifanya kazi na Conte baada ya kumsajili mshambuliaji huyo alipokuwa Inter Milan baada ya kumsajili kutoka Manchester United mwaka 2019.
Lukaku alirejea Stamford Bridge kwa kipindi cha pili katika dirisha la usajili la mwezi januari kwa kitita cha £98 million ($136m).
“Nadhani ana uwezo wa kufanya vizuri zaidi, ukiacha vyote mbinu zake. Yupo katika ubora mkubwa sana, lakini mchezaji anapaswa kuboresha kiwango chake mpaka pale atakapo staafu.” Conte aliiambia Sky Sport Italia.
“Wakati wa mchezo, kuna muda Lukaku anapaswa kurudishwa mchezoni, lakini zaidi ya hivyo ni mmoja kati ya mshambuliaji hatari kucheza dhidi yake, kwasababu anaweza kufanya hatari eneo lolote katika uwanja.
“Ukiwa na mshambuliaji kama yule, unahitaji kumtumia na sidhani kama Chelsea wameweza kutambua njia ya kumtumia mpaka sasa.” aliongeza Conte.
SPACE SPIN NA MERIDIANBET.
Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.


