Iddi Nado : Bado ni Muhimu kwa Kim Paulsen Ingawa Hachezi

Iddi Nado ananikumbusha Captain Hlompho Kekana wa Mamelodi Sundowns alijumuishwa kwenye kikosi cha AFCON 2019 cha Bafana Bafana ila bahati mbaya hakuwa akianza kwenye kikosi

Swali la kwanza la Wanahabari ni kuwa mbona muda wote alikuwa mtiifu sana mazoezini na alikuwa anahamasisha sana wenzake? Licha ya kwamba hapati nafasi kikosini

Kekana aliwajibu kuwa kuna Kekana wawili ndani ya nafsi moja! Kuna Kekana Mcheza mpira na kuna Kekana Raia wa Afrika Kusini ambaye ni Shabiki mkubwa wa taifa lake

Captain Fantastic alimaliza maneno yake ni ilikuwa rahisi kumuelewa, kama hatoanza kama Mchezaji basi atakaa kwenye bench na kuwashangilia na kuhamasisha wenzake kwa kofia ya Uzalendo na Ushabiki kwa Taifa lake

Well leo nilitulia kwenye mechi nzuri sana kati ya Taifa Stars dhidi ya Benin! Awali ya yote nilivutiwa sana na picha iliyopostiwa na kurasa rasmi za tanfootbal , macho yangu yalinasa kwa Idi Seleman Nado

Iddi Nado
Iddi Nado

Alisimama mbele zaidi kapiga goti na umakini mkubwa akimsikiliza Kocha Kim Poulsen, ni ngumu kuamini kuwa Iddi mwenyewe anajua haanzi au hatopata nafasi ila nafsi na roho yake zipo tayari kwa ajili ya taifa lake

Ananikumbusha pia alipoulizwa David Silva kwanini alikuwa makini sana kumsikiliza Kocha Del Bosque, nae akasema ni bahati kufundishwa na Kocha kama huyo pale Hispania, kama hatoanza mbele ya wakina Iniesta na Xavi basi anapata elimu ya kwenda nayo Valencia

Tukio la pili la Iddi Nado ni pale Stars inashambuliwa, nilikuwa nastream live kupitia FIFA TV! Licha ya kuwa hachezi ila sasa yeye ndie Shabiki mkubwa wa Taifa lake wakiwa ugenini, hajasomea Ukocha ila alisimama kutoa maelekezo peke yake

Iddi Nado Alisimama kuwakumbusha wenzake, licha ya kuwa hachezi ila walau maneno yake yatawasaidia kwenye mapambano kule Benin, bila kinyongo kwakuwa anafanya kwa ajili ya taifa lake


PIGA MKWANJA NA LA ROUGE

Fanya wiki yako iwe ya kuvutia zaidi, tunaelekea Los Angeles kutengeneza mkwanja na kasino maridhawa ya LA Rouge kutoka katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Fursa ya kufurahi huku unajaza pochi yako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.